Debora

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Debora alivyochorwa na Guillaume Rouillé katika Promptuarii Iconum Insigniorum.

Debora (kwa Kiebrania דְּבוֹרָה|Dvora|Dəḇôrā, yaani Nyuki), mke wa Lapidothi, alikuwa nabii na mwamuzi wa taifa la Israeli katika karne ya 12 KK.

Mwanamke jasiri, aliweza kufanya mambo mengi makubwa katika historia ya wokovu kama inavyoelezwa na Biblia katika kitabu cha Waamuzi, sura 4-5.

Kwa miaka 40 hivi (kama 1160 KK-1121 KK) aliamua Waisraeli chini ya mtende kati ya Rama na Beteli.

Aliongoza pia jeshi la makabila kadhaa ya Israeli ya Kaskazini dhidi ya Yabin, mfalme mmojawapo wa Kanaani, mwenye makao makuu huko Hazor.

Wimbo wa Debora, unaoshangilia ushindi wake katika sura ya 5, ni shairi linalohesabiwa kati ya maandishi ya zamani zaidi ya Kiebrania, ukikadiriwa kuwa uliandikwa katika karne ya 12 KK.[1]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Coogan, Michael D. (2011), The Old Testament, A Historical and Literary Introduction to the Hebrew Scriptures, Oxford University Press, pp. 214, 219 

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Debora kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.