Nenda kwa yaliyomo

Ndoa katika Uislamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ndoa katika uislam)
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Manabii
Misahafu
Malaika
Uteule
Kiyama
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalaSaumu
HijaZaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'anSunnahHadithi
Wasifu wa Muhammad
Sharia
Elimu ya Sheria za KiislamuKalam

Historia ya Uislamu

Historia
SunniShi'aKharijiyaRashidunUkhalifaMaimamu

Tamaduni za Kiislamu

ShuleMadrasa
TauhidiFalsafaMaadili
Sayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
Uchumi
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

Uislamu na dini nyingine
Hofu ya Uislamu

Ndoa katika Uislamu (kwa Kiarabu nikah) ni mapatano ya kisheria kati ya mwanamume na mwanamke. Inafungwa kwa njia ya mkataba wa ndoa ambao mara nyingi ni wa kimaandishi mbele ya mashahidi wawili na mlezi (wali) wa bibi harusi. Talaka inawezekana kwa masharti fulani. Washia wana pia ndoa ya muda (kwa Kiarabu mutʻa) ambapo muda fulani hukubaliwa kati ya wanandoa.

Katika mapokeo ya Uislamu ndoa hutiliwa moyo kwa kukumbuka tamko la mtume Mohammad: “Enyi vijana, aliye na uwezo wa kuoa aoe, kufanya hivyo kutamsaidia kuinamisha macho yake chini na kuwa mtii. Na utii ni sehemu ya imani”. (Bukhari)

Katika aya mbalimbali Qur'an inasema kuwa Mungu ameumba waume na wake ili waishi pamoja kwa mapenzi, wazae watoto na kuishi kwa amani na utulivu; kwa njia hiyo wataweza kutii amri zake na kufuata mafundisho ya Mtume wake.

Umuhimu wa ndoa katika Uislamu na jamii kwa ujumla

[hariri | hariri chanzo]

Katika Uislam ndoa ina faida kubwa na nyingi mno kwa jamii. Faida za ndoa ni kama zifuatazo:

1. Kujenga undugu katika jamii.

2. Njia halali ya kuzaliana

3. Ni kitendo cha uchaji Mungu

4. Njia mojawapo ya ibada. "Mnapokuwa katika ndoa mnakuwa mpo katika kumuabudu Mwenyezi Mungu na kufuata mwenendo wa mtume wake".

Kwa ujumla suala la ndoa ni muhimu na ni lazima kwa jamii. Maneno haya yanathibitishwa na wanazuoni kama Imamu Abu Hanifa, Ahmad bin Hanbal na Malik wanaosema, "Ingawa asili yake inaonekana ni jambo lisilokuwa la lazima, lakini kwa baadhi ya watu linakuwa ni lazima (wajibu)".

Wanazuoni wamefikia makubaliano kuwa ndoa ni lazima kwa Muislamu mwenye uwezo wa kumhudumia mke. Allah ameahidi kuwasaidia wale wenye kuoa kwa ajili ya kujikinga pale aliposema: “Waozesheni miongoni mwenu wale walio wajane na wema miongoni mwa wajakazi wenu waume au wake iwapo masikini, Allah atawatajirisha kutokana na hazina zake”. (24:32)

Wanawake wasioruhusiwa kuolewa

[hariri | hariri chanzo]

Kwa mujibu wa Uislamu, wanawake wafuatao hawaruhusiwi kuolewa na yule mtu anayehitaji kuoa.

1. Mke wa baba. Mke wa baba yako (mama) huruhusiwi kumuoa. Mke huyo awe ameachika au amefiwa na mume wake, yaani, baba yako.

2. Mama, wakiwemo mabibi wa pande zote. Mama yako mzazi na yeye pia haramu kwako. Mama yako pamoja na bibi zako wote upande wa mama na baba.

3. Binti, wakiwemo wajukuu wa kike kutokana na watoto wako wa kike au wa kiume. Ikiwa una mtoto wa kike pamoja na watoto wa mtoto wako wa kike au wa kiume (wajukuu) nao huruhusiwi kuwaoa.

4. Dada, akiwemo wa baba au mama mmoja. Dada yako ikiwa mmechanga baba au mama mmoja na yeye pia huruhusiwi kumuoa.

5. Shangazi kwa baba, au mama mmoja na baba.

6. Binti wa kaka. Yaani mwanao (mtoto wa kaka yako).

7. Binti wa dada. Mwanao, mtoto wa dada yako.

8. Mama aliyekunyonyesha. Ikiwa kuna mama ambaye alishiriki katika kukunyonyesha wakati wa utoto wako, huyo naye ni haramu kwako.

9. Mabinti wa mama aliyekunyonyesha. Watoto wa mama aliyekunyonyesha pia haramu kuwaoa.

10. Mkwe wako wa kike (mama wa mke). Mama yako mkwe, mama wa mkeo pia huruhusiwi kumuoa.

11. Ndugu wawili wa kike kuwaoa wakati mmoja. Yaani, huwezi kuwaoa mtu na dada yake.

12. Mwanamke mshirikina (anayeabudu sanamu). Ikiwa utabaini kuwa ni mshirikina, yaani, anayeabudu vitu vingine mbali na Muumba wake, huyo ni haramu kumuoa.

13. Kahaba. Mwanamke yeyote ambaye shughuli zake kubwa ni umalaya, naye ni haramu kumuoa.

Wanawake wasioruhusiwa kuchumbiwa

[hariri | hariri chanzo]

1. Mwanamke aliye katika eda.

2. Mwanamke aliyechumbiwa na mume mwingine.

Mambo yatakikanayo kutimia ili ndoa ikamilike kufungwa

[hariri | hariri chanzo]

1. Muoaji na muolewaji.

2. Mashahidi wawili.

3. Mahari (Kama zawadi kwa mwanamke).

4. Mlezi: Baba au mwakilishi wake wa kutoa idhini.

5. Kauli ya kuozesha na kukubali.