Mitume na Manabii katika Uislamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalaSaumu
HijaZaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'anSunnahHadithi
Elimu ya Sheria za KiislamuKalam
Wasifu wa Muhammad
Sharia

Historia ya Uislamu

SunniShi'aKharijiyaRashidunUkhalifaMaimamu

Tamaduni za Kiislamu

ShuleHistoria
TauhidiFalsafaSayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

Hofu ya Uislamu

Manabii wa Uislamu ni binadamu wanaume ambao huhesabiwa na Waislamu kuwa manabii waliochaguliwa na Mungu. Kwa imani ya Kiislamu manabii hao wote walihubiri ujumbe uleule wa kumwabudu Allah.

Kwenye Qur'an

Kuna majina ya watu 25 kwenye Qur'an wanaotajwa kuwa manabii. Wengi kati yao hutajwa pia katika Biblia na majina yao jinsi yalivyo kawaida katika Uyahudi na Ukristo yanatajwa katika mabano.

Sehemu za habari za manabii wa Qurani na watu wa Biblia hulingana, lakini mara nyingi ziko tofauti pia. Kwa mfano Ibrahim wa Qurani aliambiwa na Mungu kumtoa mwanawe kama sadaka lakini jina lake halitajwi, kumbe katika Biblia habari hii inasimuliwa juu ya Isaka. Dawud hutajwa na Qurani kama nabii, wakati Daudi wa Biblia ni mfalme mwenye manabii wake (hasa Gad na Nathan), ingawa anaweza kuhesabiwa kama nabii kwa sababu ya kuchangia kitabu cha Zaburi (ambacho kina utabiri mbalimbali kuhusu Yesu.

Manabii hao wa Qurani ni pamoja na:

 1. Adam (Adamu) (آدم)
 2. Idris au Idrisa (Henoko) (إدريس)
 3. Nuh (Nuhu) (نوح)
 4. Hud (هود)
 5. Saleh au Salih (صالح)
 6. Ibrahim au Ibrahimu (Abrahamu) (إبراهيم)
 7. Luut (Lut) (لوط)
 8. Ismail au Ismaili (Ishmaeli) (إسماعيل)
 9. Ishaq au Isihaka (Isaka) (إسحاق)
 10. Ya'qub au Yakubu (Yakobo Israeli) (يعقوب)
 11. Yusuf (Yusufu) (يوسف)
 12. Ayyub (Ayubu) (أيوب)
 13. Shu'aib (شعيب)
 14. Musa (Musa) (موسى)
 15. Harun au Haruni (Aroni) (هارون)
 16. Dzul-Kifli (ذو الكفل)
 17. Dawud (Daudi) (داود)
 18. Suleyman au Suleimani (Solomoni) (سليمان)
 19. Ilyas au Ilyasa (labda Eliya) (إلياس)
 20. Al-Yasa (Elisha)(اليسع)
 21. Yunus (nabii Yona) (يونس)
 22. Zakariyya (Zakaria (Injili)) (زكريا)
 23. Yahya (Yohane Mbatizaji) (يحيى)
 24. Isa (Yesu) (عيسى)
 25. Muhammad (محمد)

Mitume na Manabii

Kufuatana na mafundisho ya Uislamu katika dini zote za mbinguni ambazo Mwenyezi Mungu amewaletea wanadamu kwa njia ya Mitume na Manabii, kama dini ya Kiyahudi, dini ya Kinasara (Ukristo) na dini ya Kiislamu, hao Mitume na Manabii wametajwa katika vitabu walivyokuja navyo, na hii ni ishara moja kubwa kuwa dini hizo zina asili moja na Mwenyezi Mungu mmoja.

Mitume katika Talmud

Katika kitabu cha Wayahudi cha Talmud, Mitume wao wametajwa kama ifuatayo:

Abrahamu, Isaka, Yakobo, Mose, Haruni, Yoshua, Samueli, Solomoni, Obadia, Jehu bin Hanani, Azaria bin Odedi, Jahazieli Mlawi, Eliezeri bin Dodavahu, Hosea, Amos, Mika, Amoz (baba wa nabii Isaya), Eliya, Elisha, Yona, Isaya, Yoeli, Nahumu, Habakuki, Sefania, Uria, Yeremia, Ezekieli, Shemaia, Baruku, Neria (baba wa Baruku, Meseia (baba wa Neria), Hagai, Zekaria, Malaki yaani Ezra, Hasofer, Mordekai Bilshan, Oded (baba wa Azaria), na Hanani (baba wa Jehu)

Mitume wengine katika Biblia

Mitume wengine walitajwa katika Agano la Kale, kati yao ni: Adamu, Noah (Nuh), Yuda (Yahuda), Daudi.

Wengine tena wanatajwa katika Agano Jipya, hasa Yohane Mbatizaji (Yahya) na Yesu bin Mariamu ('Îsa).

Mitume katika Qurani

Mwenyezi Mungu ametaja Mitume na Manabii 25 katika Qurani, na katika Hadithi za Mtume Muhammad imetajwa kuwa idadi yao kwa jumla ni 124,000, katika hao 315 ni Mitume na waliobaki ni Manabii.

Kati ya hao waliotajwa ndani ya Qurani ni:

Adam, Idris, Nuh, Hud, Salih, Lut, Ibrahim, Ismail, Is-haq, Yaqub, Yusuf, Shu'aib, Ayyub, Dhulkifl, Musa, Harun, Daud, Sulaiman, Ilyas, Ilyas'a, Yunus, Zakaria, Yahya, Isa, na Muhammad.

Miongoni mwao, watano ni Mitume wakubwa ambao walipewa mitihani mingi wakawa na subira kustahimili matatizo ya umma zao. Hawa ni Nuhu, Ibrahimu, Musa, Isa na Muhammad.

Tofauti baina ya Mitume na Manabii

Mitume ni wale ambao Mwenyezi Mungu aliwatuma kwa kauma na umma mbalimbali ili kuwaelekeza njia yake na kuwaepusha na njia za upotofu za Ibilisi na Shetani.

Kumbe Manabii ni wale walioletewa ufunuo na wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili wawafahamishe watu wao kuhusu ujumbe wake.

Lakini si wote wanakubali kuwatofautisha hivyo.

Ujumbe wa Mitume na Manabii

Kadiri ya Uislamu Mitume na Manabii wote, tangu alipoletwa Adam mpaka Mtume wa mwisho kuletwa duniani, wote wamekuja na ujumbe mmoja wa kuwa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote na viumbe vyote ni Mmoja na hana mshirika, na kuwa yeyote atakayemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, basi huyo huwa amepotea na ametoka njia iliyonyoka, na malipo yake ni kutiwa motoni milele.

Marejeo

Mitume wa Kiyahudi http://en.wikipedia.org/wiki/Prophet#Judaism

Mitume wa Kikristo http://www.prophetskurds.com/00summary.htm

Mitume wa Kiislamu http://selhaj.bravehost.com/apostles.html