Nenda kwa yaliyomo

Nuhu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sadaka ya Nuhu ilivyochorwa na Daniel Maclise.

Nuhu anajulikana na kuheshimiwa katika dini ya Uyahudi, Ukristo na Uislamu kama mfano wa mwadilifu aliyeokolewa na Mungu katika safina wakati wa gharika kuu. Kadiri ya Biblia aliishi huko Mesopotamia.

Jina lake (kwa Kiebrania נח Noah, kwa Kiarabu نوح Nuhu) linatafsiriwa na Kitabu cha Mwanzo Mfariji, lakini maana ya hakika zaidi ni Anayeendeleza ubinadamu baada ya gharika.

Anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Novemba.

Katika Biblia[hariri | hariri chanzo]

Meli ya Nuhu, Zubdetü't-Tevarih. Kulingana na wasomi huria, hadithi ya mafuriko ya Gilgamesh imekopwa kutoka kwa Wababeli na kutafsiriwa tena katika Torati na katika Quran.[1][2][3]

Simulizi la gharika ni miongoni mwa yale yanayojulikana sana katika Biblia.

Katika simulizi hilo, Nuhu alifanya kazi kwa uaminifu ili kujenga safina kwa amri ya Mungu, ambamo hatimaye kuokoa familia yake na wanyama wote wa nchi kavu. Mungu aliigharikisha Dunia baada ya kusikitika kwamba ilikuwa imejaa dhambi.

Mwa 6:5-9:17 inatufundisha kwamba Mungu anachukizwa na dhambi, hivyo anataka kuondoa maovu duniani ili nchi impendeze kama alivyokusudia alipoiumba. Kwa ajili hiyo zamani za Nuhu alileta maji yafunike dunia na kuzamisha waovu. Lakini alisalimisha waadilifu katika safina kubwa ya kutosha, halafu akafunga nao agano thabiti (Eb 11:7).

Kadiri ya Mtume Petro maji yanayokusudiwa kutakasa dunia yote ni yale ya ubatizo (1Pet 3:17-22), na safina ambayo iokoe watu ni Kanisa, ambalo kadiri ya Agano Jipya ni la lazima kwa wokovu kama vile ubatizo unaotuingiza ndani yake.

Uso wa nchi ulipokwishatakaswa na maji njiwa akarukaruka akachuma tawi la mzeituni unaozaa matunda ya kutengenezea mafuta.

Njiwa akaonekana tena juu ya maji siku ya ubatizo wa Yesu ambapo alipakwa Roho Mtakatifu na kuyatia maji nguvu ya kutakasa watu (Mk 1:9-11; Tito 3:3-7). Maji na mafuta ndiyo mwanzo mpya kwa binadamu.

Mara alipotoka safinani Nuhu alimtolea Mungu sadaka iliyompendeza hata akaahidi hataangamiza tena binadamu kila anapostahili. Sadaka hiyo ni mfano wa ile ya Yesu msalabani, inayoadhimishwa katika ekaristi, ikituondolea adhabu nyingi na kutuletea huruma ya Mungu, yaani nafasi na neema ya kutubu (Tito 2:11-14). Hatimaye kutakuwa na hukumu itakayobagua waadilifu na waovu kama siku za Nuhu (Math 24:37-41).

Kwa namna hiyo, Mungu alifanya agano na Nuhu na kuahidi kutoharibu tena viumbe vyote vya Dunia kwa gharika.

Nuhu pia anaonyeshwa kama "mkulima wa udongo" aliyelima mzabibu, pia mnywaji wa zabibu hiyo. (Mwanzo 9:20-21)

Baada ya gharika, Mungu anaamuru Nuhu na wanawe: “zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi”.[4]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-01. Iliwekwa mnamo 2021-07-09.
  2. https://dergipark.org.tr/tr/download/article-file/557354
  3. https://www.icr.org/article/noah-flood-gilgamesh
  4. "Gmail". accounts.google.com. Iliwekwa mnamo 2024-05-30.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nuhu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.