Mzabibu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mzabibu
(Vitis spp.)
Mzabibu (Vitis vinifera)
Mzabibu (Vitis vinifera)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Vitales (Mimea kama mzabibu)
Familia: Vitaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mzabibu)
Jenasi: Vitis
L., 1753

Mizabibu ni spishi mbalimbali za jenasi Vitis katika familia Vitaceae; spishi kuu ni Vitis vinifera. Matunda yao huitwa zabibu ambazo hutumika kwa kutengeneza mvinyo. Mmea wa mzabibu ni mtambazi unaopanda juu ya mimea mingine au miwamba msituni, juu ya kuta katika bustani au kwa kamba shambani. Maua na matunda yamo kwa kicha.

Mzabibu katika Biblia[hariri | hariri chanzo]

Kwa kuwa mzabibu ulikuwa kilimo muhimu cha Israeli tangu watu wa taifa hilo walipohamia nchi hiyo, mti huo unatajwa mara nyingi katika Biblia hadi Agano Jipya. Hasa katika Injili ya Yohane, Yesu alijiita mzabibu wa kweli ambao waamini wake ni matawi yanayoweza kuzaa ikiwa tu yanadumu ndani ya shina na kufyonza utomvu wake.

Katika karamu ya mwisho Yesu pia alitumia divai iliyotokana na zabibu kama ishara ya damu yake iliyotakiwa kumwagwa msalabani kwa maondoleo ya dhambi.

Picha[hariri | hariri chanzo]