Nenda kwa yaliyomo

Familia (biolojia)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ngazi za uainishaji katika biolojia; ngazi ndogo za kati hazionyeshwi.

Familia ni ngazi katika uainishaji wa kisayansi wa viumbehai. Familia ya wanyama au mimea hujumlisha spishi mbalimbali zilizo karibu.

Kwa mfano paka-kaya ni spishi mojawapo pamoja na spishi 41 nyingine ndani ya familia ya Felidae inayojumlisha paka pamoja na chui, simba, tiger n.k.

Ndani ya familia kuna jenasi mbalimbali (zinazojumlisha spishi za karibu zaidi); kila familia ni sehemu ya ngazi ya juu zaidi inayoitwa oda. Familia ya Felidae (wanyama wanaofanana na paka) ni sehemu ya oda ya Carnivora yaani wanyama walanyama.

Kwa kawaida majina ya kisayansi ya kila familia huishia kwa

- "idae" kama ni familia ya wanyama au - "aceae" kama ni familia ya mimea.

Familia kubwa sana zinaweza kugawiwa katika nusufamilia; vilevile oda kubwa sana inaweza kuwa na familia za juu za kujumlisha ngazi ya familia.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Familia (biolojia) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.