Paka-kaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Paka-kaya
Paka-kaya
Paka-kaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Feliformia (Wanyama kama paka)
Familia: Felidae (Wanyama walio na mnasaba na paka)
Nusufamilia: Felinae (Wanyama wanaofanana na paka)
Jenasi: Felis
Linnaeus, 1758
Spishi: Felis catus
Linnaeus, 1758

Paka-kaya ni mnyama mdogo alaye nyama na ambaye amefugwa na binadamu tangu miaka maelfu. Paka ni mwana wa familia ya Felidae wanaojumlisha paka pamoja na gwagu (paka-pori) na spishi kubwa kama simba, chui na duma.

Asili ya paka ni paka za porini (kwa hakika paka-jangwa, F. s. lybica) walioanza kutafuta chakula karibu na makazi ya watu wa kale na kuwazoea. Watu walipenda paka kwa sababu paka hushika panya na wanyama wengine wadogo wanaoonekana ni waharibifu katika makazi ya watu. Kwa hiyo paka waliendelea kwa muda mrefu katika mazingira ya kibinadamu kama wawindaji wa panya waliolishwa na watu wakipewa mabaki ya chakula pia. Katika mazingira ya mjini paka hufugwa mara nyingi kama mnyama kipenzi hapati tena nafasi ya kuwinda.

Magonjwa ya paka[hariri | hariri chanzo]

Kwa sababu ya kuishi karibu sana na binadamu, magonjwa ya paka huenda yakaambukizwa kwa binadamu. Paka huenda akawa na virusi, bakteria, fungi au hata vimelea kama chawa ambao wataambukizwa kwa binadamu. Maradhi huenda yakawa hayaonekani kwa paka lakini akiambukizwa binadamu huwa basi yanaonekana. Magonjwa haya ni kama salmonella, kujikunakuna (cat scratch disease) na toxoplasmosis. Ili kujikinga, yafaa paka apulizwe kwa dawa na pia kupelekwa kwa daktari wa wanyama mara kwa mara.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: