Ua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Maua mbalimbali

Maua ni majani ya pekee kwenye sehemu za uzazi wa mimea. Mara nyingi huwa nje na rangi za kuvutia na kwa sababu hii maua yanapendwa pia na wanadamu kama mapambo. Katika lugha ya kila siku neno "ua/maua" linataja pia mmea wote mwenye maua.

Petali[hariri | hariri chanzo]

Majani ya nje au petali yanayoonekana vizuri pamoja na rangi yao huitwa petali. Huwa na rangi mbalimbali ili kuvuta wadudu wanaochavusha ua na hivyo kuusaidia mmea kuzaa. Yanaviringisha na kukinga viungo vya uzazi ndani yao.

Sehemu za ua
1 kombe, 2 Sepali, 3 Petali, 4 Stameni zenye chavulio na filamenti, 5 Kapeli ya stigma, staili na ovari

Viungo vya uzazi[hariri | hariri chanzo]

Viungo hivi ni kimsingi vya aina mbili:

 • stameni ni sehemu za kiume
 • Kapeli au pistili ni sehemu za kike

Stameni[hariri | hariri chanzo]

Stameni huwa na pande mbili.

  • Filamenti ni kama shina ya stameni. Juu yake kuna
  • Chavulio chenye mbelewele ambazo ni seli za kuzaa za kiume.

Kapeli[hariri | hariri chanzo]

Kapeli au sehemu ya kike huwa na sehemu tatu

  • Stigma ni uso wa kunata juu wa pistili; kazi yake ni kushika mbelewele
  • Staili inashika stigma na kupitisha mbelewele ndani yake
  • Ovari ina vyembekike ndani yake. Chembekike ni kama yai la mnyama; kikitunganishwa na na mbelewele mbegu unajitokeza.

Ovari na mbegu[hariri | hariri chanzo]

Baada ya utungishaji ua hukauka na mbegu unakua ndani ya ovari. Kwa mimea kadhaa ovari inaendelea kuwa tunda inayotunza mbegu ndani yake; kusidi la tunda ni kuvuta wanyama wanaokula tunda na kusambaza mbegu kwa njia hii.

Jinsia[hariri | hariri chanzo]

Mimea mengi huunganisha sehemu za kike na za kiume ndani ya ua moja, mfano ni ua la waridi. Kuna pia mimea yenye maua ambayo ni ama ya kike au ya kiume kwa mfano maua ya mtango au mboga.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.