Nenda kwa yaliyomo

Mbelewele

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nzi anayekaa juu ya chavulio la ua; punje ya njano ni mbelewele.
Punje za mbelewele za maua mbalimbali chini ya hadubini. Ukubwa halisi wa kichwa ni milimita 2.5.

Mbelewele (au chavua) ni punje zenye seli za kuzaa za kiume ndani ya maua. Zinapatikana kwenye chavulio juu ya stameni ya ua. Mbelewele ni lazima kwa mbegu wa mmea kujitokeza.

Mimea mingine huwa na mbelewele nyepesi inayosambazwa na upepo na kufikia kwenye kapeli ya ua.

Kuna aina nyingine zenye mbelewele nzitonzito inayonata ikiguswa. Aina hizo zina proteini na sukari, hivyo zinapendwa kama chakula cha wadudu.

Kama mdudu, kwa mfano nyuki au nzi, anafikia ua anaanza kula au kukusanya mbelewele. Wakati wa kazi hiyo punje nyingi zinanata mwilini na miguuni mwa mdudu anayezipeleka kwa maua mengine na kuzitungisha kwa njia hiy.

Nyuki hukusanya mbelewele na kuipeleka kwenye mzinga wa nyuki inapotunzwa katika vyumba vya sega. Hapa inageukia kuwa asali.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbelewele kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.