Nenda kwa yaliyomo

Sega

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sega ya asali
Nyuka hujenga vyumba vya sega kuanzia juu na kuviongeza. Baada ya kuweka asali ndani yake kila chumba chapewa kifuniko.

Sega ni nafasi ambako nyuki hutunza asali. Ina vyumba vingi vidogo vyenye umbo la pembesita. Nyuki hutengeneza sega kwa nta.

Kazi ya sega

[hariri | hariri chanzo]

Sega huwa na kazi mbili:

  1. ni chumba cha kulea jana za nyuki yaani mayai ya nyuki hutegwa humo na nyuki changa zinakua ndani yake.
  2. mahali pa kutunza akiba ya asali

Vyumba vya jana vinatengenezwa tofauti kwa sababu kuna aina tatu za nyuki katika kila mzinga wenye ukubwa tofauti:

  • vyumba vya wafanyakazi vya kawaida huwa na urefu wa milimita 10-12
  • vyumba vya dume walio wachache huwa na urefu wa 14 mm
  • vyumba vya malkia atakayetega mayai na kuwa mama wa wote huwa na urefu wa 20-25 mm na kujengwa kando la sega.

Sega za Nyigu

[hariri | hariri chanzo]

Nyigu ambao ni wadudu karibu na nyuki hutengeneza pia aina ya sega lakini wanaijenga kwa karatasi. Wachache wao hutunza pia asali.

Sega katika ufugaji wa nyuki

[hariri | hariri chanzo]

Katika ufugaji nyuki wa kisasa mzinga wa nyuki huwa na fremu ndani ambamo nyuki zinajenga sega. Fremu ya sega zinatolewa moja-moja bila kuharibu mzinga. Baada ya kuondoa asali fremu inarudishwa ilhali vyumba vya sega bado viko na nyuki zinaanza upya kujaza vyumba bila kupoteza muda wa kujenga sega mpya. Faida yake -kama ntaa haihitajiwi- ni kuongeza mavuno ya asali. Nyuki hutumia takriban kilogramu nane za asali kutengeneza kilogramu moja ya nta ama kwa njia ya kula asali au kwa njia ya kutotengeneza asali kwa kaziy a nta.

Katika ufugaji nyuki wa kienyeji mzinga wa nyuki hubomolewa wakati wa kutoa sega. Sega hizi hazilingani kwa umbo na ukubwa hazirudishwa tena.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Nta ya sega ina matumizi yake kwa kutengeneza mishumaa au sabuni. Katika nchi kadhaa asali huuzwa ndani ya sega. Wafuga nyuki hula sega yote.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sega kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sega kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.