Nenda kwa yaliyomo

Tito

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Tito askofu.
Kanisa lake huko Heraklion.

Tito ni mmojawapo kati ya viongozi wa kwanzakwanza wa Kanisa, akiwa mwenzi na mwandamizi wa Mtume Paulo, anayetajwa katika Nyaraka zake mbalimbali.

Alikuwa naye huko Antiokia akaongozana naye kwenye Mtaguso wa Yerusalemu,[1] ingawa jina lake halitajwi katika kitabu cha Matendo ya Mitume.

Kabla hajabatizwa alikuwa Mpagani, hivyo Paulo alikataa kabisa dai la kwamba atahiriwe ili aokoke.

Kadiri ya Nyaraka, baadaye alikuwa naye Efeso, akatumwa Korintho.[2]

Walikutana tena Makedonia,[3] halafu akawa kisiwani Krete ili kuimarisha uongozi wa Kanisa.[4]

Habari za mwisho ni kwamba alikwenda Dalmatia.

Agano Jipya halisimulii kifo chake.

Mapokeo yanasema Paulo alimpa daraja ya uaskofu kwa ajili ya Gortyn huko Krete, na kwamba alifariki mwaka 107, akiwa na umri wa miaka 95.

Tangu mwaka 1969, Kanisa Katoliki la Kilatini linamwadhimisha pamoja na Timotheo tarehe 26 Januari, siku inayofuata ile ya Uongofu wa Mt. Paulo, mwalimu wao.[5][6]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Wagalatia 2:1-3; Matendo 15:2
  2. 2 Korintho 8:6; 12:18
  3. 2 Korintho 7:6-15
  4. Tito 1:5
  5. Calendarium Romanum (Libreria Editrice Vaticana, 1969), uk. 116
  6. Martyrologium Romanum
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tito kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.