Nyaraka za Paulo
Nyaraka za Paulo ni maandiko ya Biblia ya Kikristo (Agano Jipya) 13 yenye mtindo wa nyaraka au barua yanayomtaja Mtume Paulo kama mwandishi.
Wataalamu wa leo hutofautiana kama kweli nyaraka hizo zote zimeandikwa na Paulo mwenyewe.
Kwa jumla saba zimetambuliwa na karibu wataalamu wote kuwa ni maandiko yake.
Kuhusu nyingine kuna maswali kwa sababu mbalimbali (kwa mfano tofauti za lugha, mkazo tofauti katika mafundisho), na wataalamu wengine hudai ya kuwa labda zimeandikwa na wanafunzi wake au na mwandishi kwa niaba ya Paulo.
Orodha ya nyaraka hizo
[hariri | hariri chanzo]Orodha yake katika Biblia inakwenda hivi, bila kujali tarehe ya utunzi, bali walengwa (kwanza jumuia, halafu watu binafsi) na urefu:
- Waraka kwa Waroma (Rum.)
- Waraka wa kwanza kwa Wakorinto (1Kor.)
- Waraka wa pili kwa Wakorinto (2.Kor.)
- Waraka kwa Wagalatia (Gal.)
- Waraka kwa Waefeso (Efe.)
- Waraka kwa Wafilipi (Flp.)
- Waraka kwa Wakolosai (Kol.)
- Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike (1Thes.)
- Waraka wa pili kwa Wathesalonike (2Thes.)
- Waraka wa kwanza kwa Timotheo (1Tim.)
- Waraka wa pili kwa Timotheo (2.Tim.)
- Waraka kwa Tito (Tit.)
- Waraka kwa Filemoni (Flm.)
Teolojia ya nyaraka hizo
[hariri | hariri chanzo]Kati ya mengi, Paulo, maarufu kama mtume wa mataifa, aliandika haya:
Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaotawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri; ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kutawala dunia hii hawaijui hata moja; maana kama wangalijua, wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu; lakini, kama ilivyoandikwa:
Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho, maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuaye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua yaliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu, Maana,
Ni nani aliyefahamu nia ya Bwana, amwelimishe?
Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. (1Kor 2:6-16).
Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. (1 Wakorintho 12:12-13).
Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha. Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri? Takeni sana karama zilizo kuu. Hivyo nawaonyesha njia iliyo bora. (1 Wakorintho 12:28-31).
Lakini labda mtu atasema, 'Wafufuliwaje wafu?' Nao huja kwa mwili gani? Ewe mpumbavu! uipandayo haihuiki, isipokufa; nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ngano au nyingineyo; lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu na mwili wake. Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki. Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali. Kuna fahari moja ya Jua, na fahari nyingine ya Mwezi, na fahari nyingine ya Nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota. Kadhalika na ufufuo wa wafu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutoharibika; hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa Roho.
Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko. Ndivyo ilivyoandikwa: mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. Lakini hautangulii ule wa Roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. Kama ilivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni. Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika.
Angalieni, nawaambia ninyi siri: Hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo ndipo litakapokuwa lile neno lililioandikwa:
Mauti imemezwa kwa kushinda. Ku wapi, ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, ewe mauti, uchungu wako?
Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni Torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo! (1 Wakorintho 15:35-57).
Basi wapendwa wangu, kama vile mlivyotii siku zote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kutimiza kusudi lake jema. Yatendeni mambo yote pasipo manung'uniko wala mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na hila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure. Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote. Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami. (Wafilipi 2:12-18).
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Aland, Kurt. “The Problem of Anonymity and Pseudonymity in Christian Literature of the First Two Centuries.” Journal of Theological Studies 12 (1961): 39–49.
- Bahr, Gordon J. “Paul and Letter Writing in the First Century.” Catholic Biblical Quarterly 28 (1966): 465–77. idem, “The Subscriptions in the Pauline Letters.” Journal of Biblical Literature 2 (1968): 27–41.
- Bauckham, Richard J. “Pseudo-Apostolic Letters.” Journal of Biblical Literature 107 (1988): 469–94.
- Carson, D.A. “Pseudonymity and Pseudepigraphy.” Dictionary of New Testament Background. Eds. Craig A. Evans and Stanley E. Porter. Downers Grove: InterVarsity, 2000. 857-64.
- Cousar, Charles B. The Letters of Paul. Interpreting Biblical Texts. Nashville: Abingdon, 1996.
- Deissmann, G. Adolf. Bible Studies. Trans. Alexander Grieve. 1901. Peabody: Hendrickson, 1988.
- Doty, William G. Letters in Primitive Christianity. Guides to Biblical Scholarship. New Testament. Ed. Dan O. Via, Jr. Philadelphia: Fortress, 1988.
- Gamble, Harry Y. “Amanuensis.” Anchor Bible Dictionary. Vol. 1. Ed. David Noel Freedman. New York: Doubleday, 1992.
- Haines-Eitzen, Kim. “‘Girls Trained in Beautiful Writing’: Female Scribes in Roman Antiquity and Early Christianity.” Journal of Early Christian Studies 6.4 (1998): 629–46.
- Kim, Yung Suk. A Theological Introduction to Paul's Letters. Eugene, Oregon: Cascade Books, 2011.
- Longenecker, Richard N. “Ancient Amanuenses and the Pauline Epistles.” New Dimensions in New Testament Study. Eds. Richard N. Longenecker and Merrill C. Tenney. Grand Rapids: Zondervan, 1974. 281-97. idem, “On the Form, Function, and Authority of the New Testament Letters.” Scripture and Truth. Eds. D.A. Carson and John D. Woodbridge. Grand Rapids: Zondervan, 1983. 101-14.
- Murphy-O’Connor, Jerome. Paul the Letter-Writer: His World, His Options, His Skills. Collegeville, MN: Liturgical, 1995.
- Richards, E. Randolph. The Secretary in the Letters of Paul. Tübingen: Mohr, 1991. idem, “The Codex and the Early Collection of Paul’s Letters.” Bulletin for Bulletin Research 8 (1998): 151–66. idem, Paul and First-Century Letter Writing: Secretaries, Composition, and Collection. Downers Grove: InterVarsity, 2004.
- Robson, E. Iliff. “Composition and Dictation in New Testament Books.” Journal of Theological Studies 18 (1917): 288–301.
- Stowers, Stanley K. Letter Writing in Greco-Roman Antiquity. Library of Early Christianity. Vol. 8. Ed. Wayne A. Meeks. Philadelphia: Westminster, 1989.
- Wall, Robert W. “Introduction to Epistolary Literature.” New Interpreter’s Bible. Vol. 10. Ed. Leander E. Keck. Nashville: Abingdon, 2002. 369-91.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Marcionite Prologues to the Pauline Epistles
- Chronological Order of Paul's Letters
- Chronology of Paul's Letters Ilihifadhiwa 28 Julai 2013 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyaraka za Paulo kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |