Ufalme wa Mungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mungu Baba juu ya kiti cha enzi[1], Westphalia, Ujerumani, mwisho wa karne ya 15.
Yesu akimpa Mtume Petro funguo za ufalme wa mbinguni (Math 16:18),[2] kadiri walivyochorwa na Pietro Perugino, 1492.
Malaika akipuliza tarumbeta ya mwisho kwa ajili ya hukumu kadiri ya 1Kor 15:52, Langenzenn, Ujerumani, karne ya 19.

Ufalme wa Mungu (au Ufalme wa mbinguni unavyoitwa hasa katika Injili ya Mathayo) ni mojawapo kati ya mada kuu za ujumbe wa Yesu Kristo katika Injili .[3] Neno "ufalme" (kwa Kigiriki βασιλεία, Basileia) linapatikana mara 162 katika Agano Jipya, kawaida kwa maana ya Basileia tou Theou (βασιλεία τοῦ θεοῦ), Ufalme wa Mungu, au Basileia tōn Ouranōn, (Βασιλεία τῶν Ουρανῶν), Ufalme wa Mbinguni.[4][5]

Hata katika hilo Agano Jipya limeendeleza Agano la Kale, ambapo Mungu anatangazwa kuwa mfalme wa ulimwengu[6][7][8] akiwa na mwakilishi, Daudi na watawala wa ukoo wake, kwa namna ya pekee Masiya, Mwana wa Daudi aliyetarajiwa.

Biblia inatangazwa kwamba hatimaye Mungu atawahukumu watu wote kadiri walivyokubali au kukataa mamlaka yake[9]. Juu ya msingi wa madondoo mbalimbali wa Agano Jipya, Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli inathibitisha kwamba hukumu hiyo itafanywa kwa njia ya Yesu. Pia kwa sababu hiyo mwenyewe alipenda kujiita "Mwana wa Mtu" kadiri ya njozi ya Danieli.

Madhehebu ya Ukristo leo yanatofautiana sana katika kuelewa na kueleza mada hiyo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Bowker 2005, pp. Throne of God entry
  2. The Gospel of Matthew (Sacra Pagina Series, Vol 1) by Dainel J. Harrington 1991 ISBN 978-0-8146-5803-1 page 248
  3. The Gospel of Matthew by R.T. France (21 Aug 2007) ISBN 080282501X pages 101-103
  4. Theology for the Community of God by Stanley J. Grenz (Jan 31, 2000) ISBN 0802847552 page 473
  5. Kingdom of God is translated to Latin as Regnum Dei and Kingdom of Heaven as Regnum caelorum. See A Primer of Ecclesiastical Latin by John F. Collins (Aug 1985) ISBN 0813206677 page 176
  6. (2005) "Kingdom of God", Dictionary for Theological Interpretation of the Bible. Grand Rapids: Baker Book House, 420–2. ISBN 978-0-8010-2694-2. 
  7. Dictionary of Biblical Imagery by Leland Ryken, James C. Wilhoit and Tremper Longman III (Nov 11, 1998) ISBN 0830814515 pages 478-479
  8. Psalms: Interpretation by James Mays 2011 ISBN 0664234399 pages 438-439
  9. "The Hebrew word malkuth [...] refers first to a reign, dominion, or rule and only secondarily to the realm over which a reign is exercised. [...] When malkuth is used of God, it almost always refers to his authority or to his rule as the heavenly King." See George Eldon Ladd, The Presence of the Future: The Eschatology of Biblical Realism, Eerdmans (Grand Rapids: 1974), 46–47.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christianity Symbol.png Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ufalme wa Mungu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.