Nenda kwa yaliyomo

Kiebrania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kiebr.)
"jisrael" ni neno "Israel" kwa lugha ya Kiebrania na kwa mwandiko wa Kiebrania

Lugha ya Kiebrania (עברית ‘Ivrit,  matamshi ya kisasa ?) ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel (pamoja na Kiarabu). Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.

Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.

Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.

Lugha za Kisemiti

[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya Kiebrania pamoja na zile za Kiarabu, Kiaramu na Kiamhari (Ethiopia) zinatokana na asili moja ya lugha ya Kisemiti. Kuna lugha nyingi ambazo zinatokana na asili hiyohiyo kama Kiashuru, Kifoinike, Kikaldayo na kadhalika.

Mwandiko wa Kiebrania

[hariri | hariri chanzo]

Makala Kuu: Mwandiko wa Kiebrania

Mwandiko wa lugha hiyo hufanywa kwa mwandiko wa pekee unaojulikana tangu miaka 3,000. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi. Tabia hii ni sawa na alfabeti nyingine za Kisemiti kama Kiaramu au Kiarabu.

Mfano: Jina la Abrahamu huandikwa "אַבְרָהָ֛ם" ambazo ni herufi "aBRHM" pekee; Alef ambayo ni herufi la kwanza tena si "a" kwa hakika. Vokali zinaweza kuonyeshwa kwa nukta na mistari chini ya herufi lakini mara nyingi haziandikwi.

Alef Bet/Vet Gimel Dalet He Waw Zayin Khet Tet Yod Kaf/Khaf
א ב ג ד ה ו ז ח ט י כ
ך
Lamed Mem Nun Samekh Ayin Pe/Fe Tsadeh Qof Resh Shin/Sin Taw
ל מ נ ס ע פ צ ק ר ש ת
ם ן ף ץ

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kiebrania kilikuwa lugha ya Israeli ya Kale wakati wa Biblia kuanza kuandikwa. Baada ya Uhamisho wa Babeli Wayahudi walianza kutumia Kiaramu, na polepole Kiebrania hakikuzungumzwa tena, lakini kilifundishwa kama lugha ya kidini. Wayahudi wa kawaida walikitumia katika ibada na wataalamu waliandika vitabu kwa lugha hiyo.

Katika karne ya 20 Wayahudi wa Ulaya waliamua kukifufua kama lugha hai. Kimekuwa lugha ya nchi mpya ya Israel tangu 1948. Watu waliohamia Israel kutoka mahali pengi duniani walijifunza Kiebrania na watoto wao wameishika kama lugha yao ya kawaida.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiebrania kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.