Nenda kwa yaliyomo

Mwandiko wa Kiebrania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kiebrania

Mwandiko wa Kiebrania ni mwandiko au alfabeti ya lugha ya Kiebrania ya kale na ya kisasa, pia ya Kiaramu ya Biblia na ya Talmudi.

Kuna pia lugha nyingine za Kiyahudi kama Kiyiddish na Kiladino zilizoandikwa kwa kutumia mwandiko huu.

Herufi[hariri | hariri chanzo]

Mwandiko huu unafuata mfumo wa abjadi yaani herufi zake zinaonyesha konsonanti pekee. Kuna herufi 22 na hakuna tofauti kati ya herufi kubwa na ndogo (kama vile A-a, B-b) lakini herufi kadhaa zina umbo tofauti kama zinaandikwa katikati au mwishoni mwa neno. Alama za א ה ו י zinaweza pia kuonyesha vokali ndefu. Vinginevyo kuna nukta zinazoweza kuandikwa juu au chini ya herufi za konsonanti kwa kuonyesha vokali.

Herufi tatu za ב bet, כ kaf na פ pe zinaweza kuonyesha sauti mbili tofauti, ama kwa matamshi laini au magumu. Hapo Bet inaweza kuwa na matamshi ya B au V, Kaf kama K au Kh na Pe kama P au F. Tofauti inaweza kuonyeshwa kwa kuweka nukta katikati ya herufi kwa kutofautisha namna hizi mbili. Mfano : b בּ / v ב .

Mwelekeo wa mwandiko ni kutoka kulia kwenda kushoto, sawa na Kiarabu na kinyume cha mwandiko wetu wa Kilatini.

Alef Bet/Vet Gimel Dalet He Waw Zayin Khet Tet Yod Kaf
א ב ג ד ה ו ז ח ט י כ
ך
Lamed Mem Nun Samekh Ayin Pe/Fe Tsadeh Qof Resh Shin/Sin Taw
ל מ נ ס ע פ צ ק ר ש ת
ם ן ף ץ

Historia[hariri | hariri chanzo]

Asili ya mwandiko wa Kiebrania ni alfabeti ya Kifinisia. Tangu karne ya 10 KK herufi za Kifinisia zilizobadilishwa kiasi zilitumiwa kuandika Kiebrania cha kale[1]. Mwandiko huu ulitumiwa wakati wa falme za Israeli na Yudah. Baada ya uhamisho wa Babeli Wayahudi walianza kutumia namna ya mwandiko wa Kiaramu (uliotoka pia kutoka Kifinisia).

Mwandiko huo uliendelea kutumiwa kwa kuandika Kiebrania katika karne nyingi ambazo Wayahudi waliishi ugenini nje ya nchi yao ya asili. Katika karne zile Kiebrania kilikuwa lugha ya kidini na ya kitaalamu lakini haikuwa tena lugha ya kwanza.

Katika karne ya 19 na ya 20 Kiebrania kilikuwa na aina ya ufufuko kama lugha ya kila siku katika harakati ya Uzayuni na hasa tangu kuundwa kwa nchi ya Israeli.

Herufi kama namba[hariri | hariri chanzo]

Herufi zilitumiwa pia kama namba ingawa hii si kawaida tena katika Kiebrania cha kisasa.

Herufi Maana ya namba Herufi Maana ya namba Herufi Maana ya namba
א 1 י 10 ק 100
ב 2 כ 20 ר 200
ג 3 ל 30 ש 300
ד 4 מ 40 ת 400
ה 5 נ 50 ך 500
ו 6 ס 60 ם 600
ז 7 ע 70 ן 700
ח 8 פ 80 ף 800
ט 9 צ 90 ץ 900

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Old Hebrew

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons

Baobonye za Kiebrania kwenye Intaneti[hariri | hariri chanzo]