Kiaramu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kiaramu ni mojawapo kati ya lugha za Kisemiti ambazo zinapangwa kati ya lugha za Afrika-Asia pamoja na Kiebrania na nyinginezo.

Inatumika tangu miaka 3,000 iliyopita. Ndiyo lugha aliyoitumia Yesu pamoja na Wayahudi wengi wa wakati wake.

Sehemu chache za Biblia ziliandikwa kwa lugha hiyo wakati ilipokuwa imeenea zaidi kwenye Mashariki ya Kati, kabla haijashindwa na Kigiriki kwanza, na Kiarabu baadaye.

Hata hivyo watu 445,000 hivi wanaitumia hata leo, hasa nchini Syria, Iraq na Uturuki.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]