Nenda kwa yaliyomo

Tanakh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tanakh ya Kiebrania; maandishi ya nje yasema "Torah - Neviim - Ketuvim"

Tanakh (תנ״ך) ni jina la Kiebrania la Biblia ya Kiyahudi.

Tanakh ni kifupi kinachounganisha herufi tatu "T" - "N" - "Kh" ambazo ni mianzo ya maneno matatu ya Kiebrania yanayotaja sehemu tatu ndani ya Biblia ya Kiebrania.

  • 1. Torah (תורה) ni Torati au vitabu vitano vya kwanza vinavyoitwa pia "vitabu vya Musa". Mara nyingi vyaitwa pia "sheria" katika imani ya Uyahudi. Hivi ni vitabu vinavyoitwa ama Kitabu cha kwanza, cha pili, cha tatu cha Musa au kwa majina yafuatayo:
    • Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati.
      • Majina ya Kiebrania ya vitabu hivi ni maneno ya kwanza ya Kiebrania ya kila kitabu: Bereshit (בְּרֵאשִית) yaani mwanzo (Hapo mwanzo..); Shemot (שְמוֹת) yaani majina (Basi majina ya wana wa Israeli...); Wayikra (וַיִּקְרָא) yaani "akaita" (Bwana akamwita Musa...); Bemidbar (בְּמִּדְבַּר) yaani "porini, nyikani" (Bwana akanena na Musa katika bara ya Sinai = nyika ya Sinai...); Devarim (דְּבָרִים) yaani "maneno" (Haya ndiyo maneno...)

Mgawanyo huo wa vitabu ni tofauti kiasi na namna ya kuvipanga katika Biblia ya Kikristo vinamopatikana katika sehemu ya kwanza ambayo inaitwa Agano la Kale na kufuatwa na Agano Jipya lililoandikwa baada ya Yesu ambaye Wakristo wanaamini ndiye Masiya aliyetabiriwa tangu kale.

Hasa Wakristo wanawauliza kaka zao Wayahudi: imekuwaje ufunuo wa Mungu kwao ulisimama tangu miaka zaidi ya 2000 ingawa wao wanamsubiri bado Masiya afike? Je, historia ya wokovu imekatika?