Kitabu cha Nahumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nabii Nahumu katika picha ya Waorthodoksi ya karne XVIII.

Kitabu cha Nahum (kwa Kiebrania נחום) ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya gombo la Manabii wadogo katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na kwa hiyo pia katika Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Muda[hariri | hariri chanzo]

Kitarehe kinashika nafasi kati ya kile cha nabii Mika na kile cha Habakuki.

Mada[hariri | hariri chanzo]

Katika kitabu hiki Nabii Nahumu anashangilia kwa ufasaha wa kishairi ujio wa maangamizi ya dola la Waashuru na ya makao yao makuu, Ninawi (612 KK): hivyo adui wa taifa na wa Mungu hatimaye ataadhibiwa.

Mtunzi[hariri | hariri chanzo]

Mtunzi anadhaniwa kuwa nabii wa Yerusalemu wakati wa mfalme Yosia wa nchi ya Yuda.

Ufafanuzi[hariri | hariri chanzo]

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Kitabu cha Nahumu katika tafsiri ya Kiswahili (Union Version)

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.