Israeli ya Kale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ramani ya Israeli ya Kale mnamo mwaka 926 wakati wa kugawiwa kwa ufalme wa pamoja
kijani nyeusi: Ufalme wa Israeli na makabila yake (kaskazini)
ijani nyeupe: Ufalme wa Yuda na makabila yake (kusini);
Philiste: nchi ya Wafilisti

Israeli ya Kale ni jina la watu au taifa walioitwa taifa teule katika Tanakh au Biblia ya Kiebrania (kwa hiyo pia katika Agano la Kale lililo sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kihistoria waliishi katika nchi iliyoitwa Kanaani, halafu Israeli (baadaye pia Palestina) kuanzia mnamo 1200 KK hadi mnamo mwaka 70 BK Waroma wa Kale walipovamia na kuharibu Yerusalemu, ambao tena mwaka 135 waliwafukuza wote kutoka nchi yao.

Wenyeji walijiita mwanzoni Wanaisraeli na baadaye pia Wayahudi.

Mwanzo na mwisho wa historia ya Israeli ya Kale[hariri | hariri chanzo]

Historia ya Israeli ya Kale inaanza tangu kupatikana kwa taifa hili katika nchi yake inayoitwa Israeli. Kufuatana na masimulizi katika Agano la Kale taifa la Israeli lilianzishwa na Wanaisraeli waliotoka Misri chini ya uongozi wa Musa na kuhamia Kanaani mnamo mwaka 1200 KK chini ya Yoshua.

Wataalamu wengine wa kisasa wanaona ya kwamba taifa lilitokea hasa ndani ya nchi kwa kuungana kwa vikundi mbalimbali.

Muungano huu wa vikundi na makabila ukawa taifa na kuunda ufalme wa kwanza wa Israeli wakati wa mfalme Sauli aliyefuatwa na Daudi na Suleimani. Baada ya kifo cha Suleimani likatokea farakano na jina la "Israeli" likatumiwa na ufalme wa kaskazini, wakati mji mkuu wa kale Yerusalemu ukaendelea kama mji mkuu wa ufalme wa Yuda.

Falme zote mbili zilishindwa katika vita na kuanzia mwaka 587 KK hapakuwa tena na dola la kujitegemea, bali eneo lilikuwa chini ya falme mbalimbali kama vile Babiloni, Uajemi na Wagiriki wa Kale.

Lakini harakati za Wamakabayo za kurudisha uhuru uliweza kuwafukuza Wagiriki na kuanzisha ufalme wa Kiyahudi kati ya 140 KK hadi 4 KK. Hata hivyo kwanzia mwaka 63 KK ufalme huu uliwekwa chini ya ulinzi wa Dola la Roma na hatimaye kugawiwa na polepole kuwa jimbo la Kiroma (tangu 70 BK).

Uvamizi wa Yerusalemu mwaka 70 BK huhesabiwa kama mwisho wa Israeli ya Kale. Wataalamu wengine wanaona tayari uvamizi wa mji wa 587 KK na Wababeli kama mwisho wa kipindi hiki na kuangalia kipindi kati ya 587 KK hadi 70 BK kama kipindi kipya.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]