Nenda kwa yaliyomo

Ugiriki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wagiriki)
Ugiriki
Ελληνική Δημοκρατία
Ellinikí Dimokratía
Kaulimbiu: Ελευθερία ή Θάνατος
(Eleftheria i thanatos - "Uhuru au mauti")
Wimbo wa taifa: Ύμνος εις την Ελευθερίαν - "Wimbo la Uhuru"
Mahali pa Ugiriki
Mji mkuu
na mkubwa
Athens
Lugha rasmiKigiriki
SerikaliJamhuri
Uhuru kutoka Milki ya Osmani
  Ilitangazwa
25 Machi 1821
  Ilitambuliwa
1829
Eneo
  Jumlakm2 131,957
Idadi ya watu
  Kadirio la 202110,678,632
  Msongamano77/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2025
  Jumla $467.59 billioni (ya 54)
  Kwa kila mtu $23,518(ya 30)
PLT (Kawaida)Kadirio la 2025
  Jumla $267.35 bilion
  Kwa kila mtu $25,756
HDI (2023) 0.908
- juu sana
SarafuEuro ()2
Majira ya saaUTC+2 EET
Msimbo wa simu+30
Jina la kikoa.gr

Ugiriki, pia Uyunani (kwa Kigiriki cha kisasa: Ελλάδα, Ellada, au Ελλάς, Ellas), rasmi kama Jamhuri ya Hellena, ni nchi iliyoko Kusini-Mashariki mwa Ulaya, ikipakana na Albania kaskazini-magharibi, Masedonia Kaskazini na Bulgaria kaskazini, na Uturuki mashariki. Kwa upande wa kusini na magharibi, imezungukwa na Bahari ya Mediterania, Bahari ya Aegean, na Bahari ya Ionia. Ina idadi ya watu takriban milioni 10.4, ikiwa ya 87 duniani. Mji wake mkuu na mkubwa zaidi ni Athens. Ugiriki imegawanyika katika majimbo 13 ya kiutawala. Inajulikana kwa historia yake ndefu ya ustaarabu wa kale, hasa Dola ya Kigiriki na michango yake katika demokrasia, falsafa, na sanaa. Pia ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na NATO.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Kijiografia huwa na sehemu za Ugiriki bara, rasi ya Peloponesi upande wa kusini inayounganishwa kwa shingo ya nchi nyembamba, halafu visiwa vingi upande wa Bahari ya Aegean, Bahari ya Adria na kwenye Mediteranea yenyewe. Visiwa vikubwa zaidi ni Kreta, Euboea, Lesbo na Rhodos.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Parthenon, katika Akropoli ya Athens, ni kielelezo cha Ugiriki wa Kale.

Ugiriki ni nchi yenye historia ndefu na maarufu sana, hata inaitwa "nchi mama ya Ulaya" na kitovu cha Ustaarabu wa magharibi, kwa sababu ndipo vilipoanza demokrasia, falsafa ya magharibi, fasihi ya magharibi, historiografia, sayansi ya siasa, tafiti za sayansi na hisabati, tamthilia na michezo ya Olimpiki.

Ugiriki ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 1981.

Lugha ya Kigiriki inaendelea kuandikwa kwa Alfabeti ya Kigiriki inayotumiwa tangu miaka 3000 iliyopita, lakini lugha yenyewe imebadilika. Wagiriki wa leo hawaelewi tena Kigiriki cha Kale moja kwa moja.

Wakazi wengi wanafuata dini ya Ukristo (93%), hasa katika Kanisa la Kiorthodoksi la Kigiriki (90%), halafu Waprotestanti na Wakatoliki. 2% ni Waislamu.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ugiriki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.