Georgia (nchi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
საქართველო
Georgia
Bendera ya Georgia Nembo ya Georgia
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: ძალა ერთობაშია(Kigeorgia)
"Nguvu ni Umoja"
Wimbo wa taifa: Tavisupleba ("Uhuru")
Lokeshen ya Georgia
Mji mkuu Tbilisi
41°43′ N 44°47′ E
Mji mkubwa nchini Tbilisi
Lugha rasmi Kigeorgia (pia Kiabkhazi katika Abkhazia)
Serikali Jamhuri
Mikheil Saakashvili
Nikoloz Gilauri
Chanzo cha Taifa
Kuanzishwa kwa Kolkhis
na Iberia ya Kaukazi
kama falme za kwanza katika Georgia
Ufalme wa Georgia uliounganishwa
Jamhuri ya kwanza ya Georgia
Uhuru kutoka Umoja wa Kisovyeti
Ilitangazwa
Ilitambuliwa
Ilikamilishwa

mnamo2000 BC


1008
26 Mei 1918

9 Aprili 1991
6 Septemba 1991
25 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
69,700 km² (ya 121)
Idadi ya watu
 - 2013 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
4,935,880[1] (ya 1191)
70.8/km² (137)
Fedha Lari (ლ) (GEL)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
MSK (UTC+3)
MSD (UTC+4)
Intaneti TLD .ge
Kodi ya simu +995

-

1 Population figure excludes Abkhazia and South Ossetia.


Ramani ya Georgia

Georgia (kwa Kigeorgia: საქართველო "Sakartvelo") ni nchi ya Kaukazi kati ya Ulaya na Asia kwenye mwambao wa Bahari Nyeusi. Imepakana na Urusi, Uturuki, Armenia na Azerbaijan.

Georgia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti lakini imekuwa nchi huru ya kujitegemea tangu 1991.

Mji mkuu ni Tbilisi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Georgia ni hasa nchi ya milima ya Kaukazi inayofikia kimo cha mita 5,068. Kati ya safu mbili za milima kuna tambarare ya Kolkhis.

Upande wa magharibi unaathiriwa na Bahari Nyeusi: una hali ya hewa poa na mvua nyingi inayofaa kwa kilimo hasa cha mizabibu.

Maeneo ya Abkhazia na Ossetia ya Kusini yamedai uhuru na kwa sasa hayapo chini ya serikali kuu.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Georgia ina wakazi milioni 4.5. Zaidi ya milioni 1 hukaa mjini Tbilisi.

Wakazi walio wengi (71%) husema Kigeorgia lakini kuna vikundi vya wasemaji wa Kirusi (9%), Kiarmenia (7%), Kiazeri (6%) na lugha nyingine.

Wageorgia wengi ni Wakristo wanaofuata Kanisa la Orthodoksi la Georgia (83.9%). Kuna pia wafuasi wa Kanisa la Kitume la Armenia (3.9%) na Wakatoliki (0.8%). Waislamu ni 9.9%, wakati Wayahudi wanazidi kuhama.

Watu maarufu[hariri | hariri chanzo]

Mgeorgia anayejulikana zaidi duniani alikuwa Josef Stalin, mtawala wa Urusi wakati wa Ukomunisti.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.


WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Georgia (nchi) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Georgia (nchi) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.