Turkmenistan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Türkmenistan
Turkmenistan
Bendera ya Turkmenistan Nembo ya Turkmenistan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: Wimbo la taifa huru na huria
Lokeshen ya Turkmenistan
Mji mkuu Ashgabat
37°58′ N 58°20′ E
Mji mkubwa nchini Ashgabat
Lugha rasmi Kiturkmen
Serikali Udikteta
Gurbanguly Berdimuhammedow
Uhuru
Ilitangazwa
Ilitambuliwa

27 Oktoba 1991
8 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
488,100 km² (ya 52)
4.9
Idadi ya watu
 - Desemba 2006 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
5,090,000 (ya 113)
9.9/km² (ya 208)
Fedha Manat (Turkmenistan) (TMM)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
TMT (UTC+5)
(UTC+5)
Intaneti TLD .tm
Kodi ya simu +993

-Turkmenistan ni nchi ya Asia ya Kati. Jina limetokana lugha ya Kiajemi lamaanisha "nchi wa Waturkmeni". Hadi 1991 ilikuwa jamhuri ya Umoja wa Kisovyet kwa jina la Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kimturkmeni. Imepakana na Afghanistan, Uajemi, Uzbekistan, Kazakhstan na Bahari Kaspi. Wakazi walio wengi ni Waislamu; kuna kadirio ya Waislamu asilimia 87 kati ya wakazi wote lakini haijulikani ni wangapi wanaofuata dini yao.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Map of Turkmenistan

Nchi ina eneo la 488,100 km²) karibu sawa na Kamerun. Sehemu kubwa (80 %) ni jangwa hasa jangwa Karakum. Milima ya Kopet Dag katika kusini magharibi inafikia kimo cha 2,912 m.Kati ya mito mikubwa ni Amu Darya, mto Murghab na mto Hari Rud.

Hali ya hewa haina baridi sana lakini kuna joto kali wakati wa kiangazi. Mvua ni kidogo zanyesha hasa kati ya Januari na Mei.

Miji muhimu ni Ashgabat, Turkmenbashi (zamani Krasnovodsk) na Dashoguz.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Turkmenistan ilitwaliwa na Urusi tangu mwisho wa karne ya 19 ikaingia hivyo katika Umoja wa Kisovyeti baada ya 1917 na kuwa jamhuri ndani yake. Wakati wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti kiongozi wa chama cha kikomunisti Saparmirat Niyasov akaendelea kushika uongozi akitawala kama rais hadi kifo chake mwaka 2006. Niyasov alibadilisha utawala wa chama cha kikomunisti kuwa udikteta wake yeye mweyewe. Akaanza kutumia jina la "Turkmenbashi" (Baba wa Turkmeni wote) na sanamu zake zikasimamishwa kote nchini mara nyingi sanamu za dhahabu hata kama wanachi walikuwa na maisha magumu.

Mapato kutoka gesi na mafuta ya petroli zilimwezesha kuendesha uchumi wa nchi kwa hiari yake bia mabadiliko makubwa jinsiilivyokuwa kawaida wakati wa anguko la ukomunisti penginepo. Zaidi ya nusu ya wannachi hawana ajira na kuishi maisha ya umaskini lakini wanapewa chumvi, umeme na maji bure. Mkate na petroli zinauzwa kwa bei ya duni sana lakini kuba uhaba wa mara kwa mara.

Baada ya kifo cha Niyasov kamati ya viongozi ilimteua makamu wa waziri mkuu Gurbanguly Berdimuhammedov kuwa rais mpya ingawa kikatiba mwenyekiti wa bunge alitakiwa kuchukua nafasi hii. Mwenyekiti wa bunge alishtakiwa mbele ya mahakama juu ya makosa fulani na Berdimuhammedov alithebitishwa katika uchaguzi wa 11 Februari 2007 kwa 89% za kura. Watazamaji walidai kura ilikuwa ya uwongo.

BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Turkmenistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.