Kiajemi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la Kiajemi

Kiajemi (au Kifarsi, فارسی; au Kiparsi, (پارس) ni lugha ya taifa ya Uajemi. Ni kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi, ambazo tena ni kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Inaandikwa kwa herufi za Kiarabu ambamo herufi nne za ziada zimeongezwa kwa kutaja sauti zisizoweza kuonyeshwa kwa Kiarabu asilia. Hizo herufi za ziada ni پ p, چ ch, ژ zh na گ g.

Kiajemi kilikuwa na athira kubwa juu ya lugha mbalimbali hasa Kiarabu na Kituruki, lakini pia Kiswahili.

Kuna wasemaji wa lugha ya kwanza milioni 70, na takriban wasemaji wengine milioni 60 kama lugha ya pili. Inatumiwa hasa katika nchi zifuatazo:

  • Katika Afghanistan, yenye wasemaji takriban milioni 15, lugha inaitwa "Kidari" (درى).
  • Katika Tajikistani, yenye wasemaji milioni 15 pia, lugha inaitwa "Kitajiki".

Kutokana na uhamiaji wa karne ya 20 lugha inapatikana katika nchi nyingi za dunia.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]