Kitajiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lugha za Kiirani; maeneo penye wasemaji wa Kitajiki pamoja na Kiajemi yana rangi ya kijani-nyeupe

Kitajiki (тоҷикӣ / تاجیکی / tamka "tojiki" au забони тоҷикӣ / زبان تاجکی / tamka "zabone tojiki") ni lugha rasmi nchini Tajikistan katika Asia ya Kati. Kuna pia wasemaji wa Kitajiki katika Urusi na katika Uzbekistan.

Kitajiki kinatajwa mara nyingi kama lahaja ya Kiajemi. Wasemaji wa Kitajiki wanaelewana bila matatizo na wasemaji wa Kiajemi nchini Uajemi au wasemaji wa Kidari nchini Afghanistan.

Kama Kiajemi ni mojawapo ya lugha za Kiirani kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Lugha huandikwa katika Tajikistan kwa herufi za Kikyrili kama Kirusi. Hadi miaka ya 1920 iliandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]