Herufi za Kiarabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
"al-ABJaDiya al-arabiya" ni namna ya Kiarabu ya kusema "ABC xa Kiarabu"
(A-B-J-D ni herufi nne za kwanza za alfabeti ya Kiarabu)

Herufi za Kiarabu ni maandishi ya lugha ya Kiarabu. Nje ya Kiarabu lugha mbalimbali zinaandikwa kwa herufi za kiarabu hasa lugha za nchi penye Waislamu wengi. Kati ya lugha hizi ni Kiajemi, Kikurdi, Kimalay na Urdu. Kihistoria hata Kiswahili na Kituruki ziliwahi kuandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Kuna herufi 28 za Kiarabu zinazoandikwa kutoka upande wa kulia kwenda kushoto. Herufi zote isipokuwa sita zinaunganishwa wakati wa kuandika. Kutokana na tabia hiyo kila herufi inaweza kuonekana kwa umbo tofautitofauti kiasi kutegemeana na mahali pake mwanzoni, katikati au mwishoni mwa neno.

Kwa kawaida maandishi ya Kiarabu ni ya konsonanti tu bila vokali. Vokali zikiandikwa zinaonekana kama mstari au nukta chini au juu ya herufi zinazoanzisha sillabi.


Herufi kuu[hariri | hariri chanzo]

Umbo la herufi Jina Soma kama Alama ya matamshi ya kimaitifa
peke yake mwanzoni katikati mwishoni
أ, إ, ؤ, ئ
hamza ’ ‚ [ʔ]
alif ā [aː]
bāʾ b [b]
tāʾ t [t]
ṯāʾ th [θ]
ǧīm / j [ʤ]
ḥāʾ [ħ]
ḫāʾ / ẖ / kh [x]
dāl d [d]
ḏāl ḏ / dh [ð]
rāʾ r [r]
zāy z [z]
sīn s [s]
šīn š / sh [ʃ]
ṣād [sˁ]
ﺿ ḍād [dˁ], [ðˤ]
ṭāʾ [tˁ]
ẓāʾ [zˁ], [ðˁ]
ʿayn ʿ / ‘ [ʔˤ]
ġayn ġ / gh [ɣ]
fāʾ f [f]
qāf q / ḳ [q]
kāf k [k]
lām l [l]
mīm m [m]
nūn n [n]
hāʾ h [h]
wāw w [w]
yāʾ y [j]