Lahaja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainika kijamii au kijiografia. Lahaja za lugha moja zatofautiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati. Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa lafudhi na siyo lahaja. Uchambuzi na uchanganuzi wa lahaja ni tawi la isimujamii.

Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo:

  1. vipengele vya sera (lahaja rasmi na lahaja sanifu)
  2. vipengele vya maoni ya wasemaji wa lugha husika
  3. vipengele vya kijamii (lahaja jamii na lahaja tabaka)
  4. vipengele vya eneo

Mfano wa lugha yenye lahaja mbalimbali ni Kiingereza na lahaja zake zinavyozungumzwa tofauti Uingereza, Marekani, Uhindi, Australia na maeneo mengine. Tena, lahaja za Kiswahili hutofautishwa kulingana na maeneo yake kama Kiamu (kisiwani kwa Lamu), Kimvita (mjini kwa Mombasa), Kiunguja (kisiwani kwa Zanzibar, Kingazija (visiwani kwa Komoro) na kadhalika.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Buliba, Aswani, Kimani Njogu & Alice Mwihaki 2006, "Isimujamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili", Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lahaja kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.