Uzbekistan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
O‘zbekiston Respublikasi
O‘zbekiston Jumhuriyati
Ўзбекистон Республикаси

Jamhuri ya Uzbekistan
Bendera ya Uzbekistan Nembo ya Uzbekistan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: Wimbo la Taifa
Lokeshen ya Uzbekistan
Mji mkuu Tashkent
41°16′ N 69°13′ E
Mji mkubwa nchini Tashkent
Lugha rasmi Kiuzbeki
Serikali Jamhuri
Islom Karimov
Shavkat Mirziyoyev
Uhuru

Ilitangazwa
Formation
Recognized
Completed
1747 kama Dola la Bukhara,
Dola la Kokand, Khwarezm
1 Septemba 1991
8 Desemba 1991
25 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
447,400 km² (ya 56)
4.9
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
26,593,000 (ya 44)
59/km² (ya 136)
Fedha Som ya Uzbekistan (UZS)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
UZT (UTC+5)
not observed (UTC+5)
Intaneti TLD .uz
Kodi ya simu +998

-


Tajiks of Uzbekistan.PNG

Uzbekistan ni nchi ya Asia ya Kati. Mji mkuu na pia mji mkubwa ni Tashkent.

Imepakana na Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Turkmenistan. Kuna takriban wakazi 26,600,000.

Watu walio wengi (zaidi ya 70 %) hutumia lugha ya Kiuzbeki ambacho ni kati ya lugha za Kiturki. Kuna vikundi vingi vidogo zaidi vya utamaduni tofauti kama vile Warusi (5,5 %), Watajiki (5,1 %), Wakazakhi (4,2 %), Watartari (2 %), Wakarakalpaki (2 %), Wakorea (1,1 %) na mengine.

Hadi mwaka 1991 Uzbekistan ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet. Ilijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiuzbeki" hadi 1991.

Madrasa ya "Sherdor" mjini Samarkand

Historia[hariri | hariri chanzo]

Uzbekistan ni nchi ya historia ndefu. Ferghana, Tashkent, Bukhara, Khwarezm na Samarkand zilikuwa vitovu vya utamaduni wa kibinadamu tangu milenia ya pili KK. Katika karne kabla na baada ya Kristo eneo lilijulikana kama Sogdiana na Baktria. Miji yake ilikuwa na utajiri kutokana na biashara ya misafara kwenye barabara ya hariri kati ya China na Mashariki ya Kati.

Baadaye ilitawaliwa na milki mbalimbali za nje kama Uajemi. Kuanzia uenezi wa Uislamu watu ba Uzbekistan waligeukia dini hii mpya. Katika karne ya 14 jemadari Timur alijenga milki kubwa na kuharibu nchi za magharibi hadi Uturuki. Alipamba mji mkuu wake Samarkand kwa majengo mazuri.

Baada ya Timur milki yake iliporomoka na Uzbekistan ilitawaliwa na madola mbalimbali ya kieneo yaliyokuwa hasa eneo la mji muhimu.

Katika karne ya 19 Urusi ulieneza athira yake kuelekea kusini na kuunganisha madola ya Uzbekistan na milki yake.

Baada ya mapinduzi ya Urusi ya 1917 Uzbekistan ikawa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi kuporomoka kwake 1991.

BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uzbekistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.