Washia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nchi za Waislamu wengi na madhehebu
Kibichi: Wasunni wengi; Nyekundu: Washia wengi
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Manabii
Misahafu
Malaika
Uteule
Kiyama
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalaSaumu
HijaZaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'anSunnahHadithihttps://sw.wikipedia.org/w/index.php?search=Ali%20ibn%20Abu%20Talib&title=Maalum%3ATafuta&wprov=acrw1_2
Wasifu wa Muhammad
Sharia
Elimu ya Sheria za KiislamuKalam

Historia ya Uislamu

Historia
SunniShi'aKharijiyaRashidunUkhalifaMaimamu

Tamaduni za Kiislamu

ShuleMadrasa
TauhidiFalsafaMaadili
Sayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
Uchumi
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

Uislamu na dini nyingine
Hofu ya Uislamu

Washia (pia: Shi'a; kutoka Kiarabu:شيعة[1]) ni dhehebu katika Uislamu (Kiarabu: الإسلام). Kufuatana na makadirio mbalimbali kati ya asilimia 10 na 20 za Waislamu wote hufuata Shia na wengine walio wengi ni Wasunni.

Lakini katika nchi za Uajemi, Azerbaijan, Iraki, Bahrain, Yemen, Omani na Lebanoni Washia ndio kundi kubwa.

Tofauti kubwa kati ya madhehebu mawili hayo ni juu ya suala la uimamu au ukhalifa baada ya Mtume; hata hivyo, wana tofauti juu ya masuala mengine ya kiitikadi na hukumu pia.

Waislamu wa shia wanaamini kwamba hakuna uwongo au makosa katika Qur'an na imebakia bila kubadilika tangu kuteremshwa kwake. Hadithi inajumuisha hotuba na matendo ya Mtume na Maimamu yanayopitishwa kwetu kwa njia ya maandishi kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Neno Shia linatokana na Kiarabu shiá't ali (شیعته علی) yaani "chama cha Ali" likimaanisha kundi la wafuasi wa Ali ibn Abu Talib aliyekuwa mkwe wake Mtume Muhammad na familia yake. Dhehebu hili linashikilia na kuamini kwamba Mtume alimteua Ali kama Wasii wake (Khalīfa) na Uimamu (mafundisho ya Shia) (kiongozi wa kiroho na kisiasa) baada yake.[2] Uteuzi huo ulifanyika katika tukio la Ghadir Khumm, lakini alizuiwa kumrithi Muhammad kama kiongozi wa Waislamu kama matokeo ya chaguo lililofanywa na baadhi ya masahaba wengine wa Muhammad (ṣaḥāba) pale Saqifah.

Mtazamo huo kimsingi unapingana na ule wa Uislamu wa Kisunni, ambao wafuasi wake wanaamini kwamba Muhammad hakuteua mrithi kabla ya kifo chake na wanamchukulia Abu Bakr, ambaye aliteuliwa kuwa khalifa na kundi la Waislamu wakuu pale Saqifah, kuwa khalifa wa kwanza halali (rāshidūn) baada ya Muhammad.[3]

Chanzo cha Shia[hariri | hariri chanzo]

Washia huamini ya kwamba familia ya Muhammad hustahili kuwa na uongozi kati ya Waislamu. Familia hii huitwa "ahl-al-bayt" (Kiarabu:أهل البيت).

Ali alimwoa mtoto wa pekee wa mtume aliyeishi yaani binti yake Fatima akawa pia baba wa Hassan na Husain wajukuu wa pekee wa mtume. Baada ya kifo cha Ali wafuasi wake walitaka Hasan na Husein kumfuata katika nafasi ya uongozi wa Uislamu wote lakini idadi kubwa ya Waislamu walishikamana na Muawiya

Washia huamini ya kwamba uongozi wa ahl-al-bayt uliendelea kupitia maimamu mbalimbali.

Vikundi[hariri | hariri chanzo]

Washia waligawanyika baada ya imamu wa sita Ismail ibn Dschafar kuhusu swali ni nani imamu halali wa saba. Kutokana na farakano hili vikundi mbalimbali vilijitokeza.

  • Ithnashari: ni kundi kubwa kati ya Washia wakiwa hasa Uajemi, Iraki, Azerbaijan na Lebanoni. Huamini ya kwamba imamu wa 12 alichukuliwa na Allah na kwa sasa yuko bila kufa au bila kuonekana.
  • Waismaili waliachana juu ya imamu wa saba. Kati yao wamegawanyika tena
    • Wanizari huamini ya kwamba maimamu wameendelea hadi leo na kiongozi wao ni Aga Khan. Karim Aga Khan IV kwao ni imamu wa 49 tangu mtume Muhammad.
    • Wabohra walioko Uhindi, Pakistan na Yemen huamini ya kwamba imamu wa saba alipotea kwa sababu amechukuliwa na Mungu na yuko bila kuonekana. Imani hii hufanana kiasi na mafundisho ya Ithnashari.

Kutokana na uhamiaji wakati wa karne ya 19 matawi ya Waismaili yamepatikana pia katika Afrika ya Mashariki. Hasa Wakhodja wamejitolea katika mazingira wanapoishi kwa kujenga shule, sahanati na mahospitali vinavyoitwa mara nyingi "Aga Khan".

Kihistoria palikuwa na vikundi vingi vingine kama vile Wafatima waliotawala Misri kati ya 953 na 1171 BK.

  • Wazaidiya ni kundi la Washia walioko Yemen. Waliachana na Washia wengine juu ya imamu wa tano.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Ibn Mandhur, Muhammad b. Mukarram. Lisān al-'Arab. Qom: Adab al-Hawza, 1405 AH.
  • Izutsu, Toshihiko. Khudā wa insān dar Qur'an. Imetafsiriwa kwa Kiajemi na Ahmad Āram. Tehran: Nashr-i Farhang-i Islāmī, 1374 Sh.
  • Muṣtafawī, Hasan al-. Al-Tahqiq fi kalimat al-Qur'aan. Tehran: Wizarat-i Farhang wa Irshad-i Islāmī, 1374 Sh.
  • Nar, Sayyid Ḥusayn al-. Ramānhā wa wāqiʿīyyathā-yi Uislamu. Ilitafsiriwa kwa Kiajemi na Raḥmati. Tehran: Jāmi, 1382 Sh.
  • Riyshahrī, Muhamad. Mīzan al-Hikma. Qom: Dār al-Hadith, 1389 Sh.Subḥānī, Ja'far. Muḥāḍirāt fi al-Ilāhīyāt. Qom: Muʾassisa-yi Imām Ṣādiq, [n.d].
  • Ṭabāṭabātī, Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzan fi tafsīr al-Qur'an. Qom: Daftar-i Nashr-i Islāmi, 1417 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. Al-Hasan. Majma' al-bayan fisir al-Qur'an. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1406 AH.
  • Ṭurayḥī, Fakhr al-Dīn. Majma' al-baḥrayn. Tehran: Murtaḍawī, 1375 Sh.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Sunnis and Shia: Islam's ancient schism", BBC News, 2016-01-04. (en-GB) 
  2. Olawuyi, Toyib (2014). On the Khilafah of Ali over Abu Bakr. p. 3. ISBN 978-1-4928-5884-3. Archived from the original on 22 April 2016.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  3. The Shura Principle in Islam – by Sadek Sulaiman.