Saumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Saumu ni tendo la kujinyima chakula kwa sababu za kidini, ili kuweka roho huru kutoka utawala wa mwili wake, iweze kuinuka kwa Mungu na kutafakari kwa urahisi zaidi. Kuna pia malengo mengine ya saumu, kama vile kushikamana na mafukara.

Karibu dini zote zinafundisha umuhimu wa saumu, lakini namna ya kufunga chakula ni tofauti.

Uyahudi, madhehebu mengi ya Ukristo na hasa Uislamu vina siku maalumu za toba zinazodai kufunga.

Waislamu wanapaswa kufunga chakula na kinywaji kuanzia alfajiri hadi magharibi mwezi mzima wa Ramadhani.

Yesu, aliyefunga jangwani siku arubaini mfululizo, aliwaelekeza wafuasi wake hasa namna ya kufunga, akiwadai wasijitafutie sifa kwa binadamu wenzao. Katika Matendo ya Mitume tunaweza kusoma juu ya mafungo yaliyoendana na sala katika jumuia za kwanza za Kanisa.