Hadithi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Hadithi ni sehemu ya fasihi. Hasa kuna aina mbili za hadithi:

  • hadithi za kubuni,
  • hadithi za kihistoria.

Hadithi za kubuni[hariri | hariri chanzo]

  1. Ngano za mazimwi: Wahusika wakuu huwa mazimwi ambao hupewa sifa zinzowatenga na binadamu wengine wa kawaida.
  2. Ngano za mashujaa: Husimulia visa na vitendo na matukio ya kishujaa yanayohuhusiana na shujaa wa jamii fulani.
  3. Ngano za usuli: Hutoa asili au chanzo cha jambo.
  4. Hekaya: Hizi ni hadithi za kijanja...mhusika mmoja rafiki wa wengine hupitia njia ya ila na ujanja.
  5. Ghurufa: Wahusika huwa wanyama waliowakilisha wanadamu wenye sifa za wanadamu hao.
  6. Ngano za kimafumbo: Huwa na mafumbo yenye maana nyingine ya ndani.