Lebanoni
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Kūllūnā li-l-waṭan (Kiarabu) "Sisi sote kwa ajili ya taifa" | |||||
Wimbo wa taifa: Kulluna lil-watan | |||||
Mji mkuu | Beirut | ||||
Mji mkubwa nchini | Beirut | ||||
Lugha rasmi | Kiarabu(na zamani Kifaransa) | ||||
Serikali | Jamhuri Michel Aoun (ميشال عون) Najib Mikati (نجيب ميقاتي) | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa |
26 Novemba 1941 22 Novemba 1943 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
10,452 km² (ya 166) 1.8 | ||||
Idadi ya watu - 2015 kadirio - Msongamano wa watu |
5,851,000 (ya 112) 560/km² (ya 21) | ||||
Fedha | Lira ya Lebanon (LL) (LBP )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EET (UTC+2) EEST (UTC+3) | ||||
Intaneti TLD | .lb | ||||
Kodi ya simu | +961
- |
Lebanoni (kwa Kiarabu: لبنان ) ni nchi ndogo ya Mashariki ya Kati katika Asia ya Magharibi kando ya Bahari ya Mediteranea.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Kuna kanda nne za kijiografia:
- Kiini cha nchi ni safu ya milima ya Lebanoni inayopanda hadi kimo cha m 3000 na kuelekea sambamba na pwani ya Mediteranea.
- Kuna kanda jembamba la pwani kati ya milima na bahari.
- Upande wa mashariki kwa milima kuna tambarare ya Beka'a inayofaa kwa kilimo
- Safu ya milima ya Lebanoni ndogo mpakani kwa Syria
Mto mrefu ni Litani wenye mwendo wa km 140 unaoishia baharini karibu na mji Tyros (Sur).
Miji
[hariri | hariri chanzo]Miji mikubwa ni (kadirio ya idadi ya wakazi kwa mabano):
Historia
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kusambaratika kwa milki ya Waturuki Waosmani kutokana Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia, Lebanoni iliwekwa na Shirikisho la Mataifa iwe chini ya usimamizi wa Ufaransa.
Nchi hiyo ilipokuwa chini ya Ujerumani wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Lebanoni ilijitangazia uhuru wake mwaka 1943.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Zaidi ya nusu ya wakazi hukaa katika rundiko la jiji la Beirut.
Wenyeji wana damu mchanganyiko sana, lakini lugha ya kawaida na lugha rasmi ni Kiarabu.
Kati ya nchi za Waarabu Lebanoni ni nchi pekee yenye wakazi wengi ambao ni Wakristo wa madhehebu mengiː walau ilikuwa hivyo hadi miaka ya karibuni, kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuzuka.
Ni kwamba zaidi ya nusu ya Walibanoni wote wamehamia nje ya nchi, wakiwemo hasa Wakristo.
Kinyume chake, nchi imewapokea wakimbizi zaidi ya milioni 1.
Makadirio ya mwaka 2014 yanadai kwa sasa 54% ni Waislamu (27% Wasuni na 27% Washia), 40.5% ni Wakristo (21% Wakatoliki Wamaroni, 8% Waorthodoksi Wamelkiti, 5% Wakatoliki Wamelkiti, 1% Waprotestanti), 5.6% ni Wadruzi n.k.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Lebanon Ilihifadhiwa 11 Aprili 2011 kwenye Wayback Machine. الجمهورية اللبنانية
- Lebanon Lebanon – Country Profile
- Lebanon entry at The World Factbook
- Lebanoni katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of Lebanon
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Lebanoni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |