Milima ya Lebanoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mti wa mwerezi kwenye milima ya Libanoni

Milima ya Lebanoni ni safu ya milima katika katika nchi ya Lebanoni inayoanza katika Syria. Inaelea sambamba na pwani la Mediteranea na milima ya Lebanoni ndogo. Mwelekeo wa safu ni kutoka kaskazini kwenda kusini kwa urefu wa kilomita 240. Kilomita 160 ziko ndani ya Lebanoni na kilomita 80 ndani ya Syria.

Upande wa magharibi kuna tambarare nyembamba kando la pwani ya bahari na upande wa mashariki ni bonde la Beka'a na ngambo yake ni safu ya Lebanoni ndogo.

Sehemu ya juu ni mlima Qurnat as Sawd mwenye kimo cha mita 3,088 juu ya UB. Kuanzia mwezi wa Novemba hadiA prili milima ya juu hufunikwa na theluji iliyosababisha milimu kuitwa "leban" yaani nyeupe.

Zamani palikuwa na misitu minene lakini miti imekatwa tangu nyakati za kale na leo hii ni miti michache iliyobaki. Taarifa nyingi za Biblia zinataja miti ya Lebanoni iliyotumiwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, hekalu ya Yerusalemu na pia kwa meli. (kwa mfano Wafalme I 5,20 au Ezekieli 27,5). Mti maarufu ya Libanoni ni mti wa mwerezi.

MIlima ilikuwa kibilio kwa vikundi vingi vilivyoteswa penginepo kwa mfano Wakristo Wamaroni au Waislamu Washia na Wadruzi.

Mti wa mwerezi kutoka milima ya Lebanoni ni nembo la kitaifa ya nchi ya Libanoni