Wasunni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wasuni)
Nchi za Waislamu wengi na madhehebu
Kibichi: Wasunni wengi; Nyekundu: Washia wengi
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Manabii
Misahafu
Malaika
Uteule
Kiyama
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalaSaumu
HijaZaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'anSunnahHadithihttps://sw.wikipedia.org/w/index.php?search=Ali%20ibn%20Abu%20Talib&title=Maalum%3ATafuta&wprov=acrw1_2
Wasifu wa Muhammad
Sharia
Elimu ya Sheria za KiislamuKalam

Historia ya Uislamu

Historia
SunniShi'aKharijiyaRashidunUkhalifaMaimamu

Tamaduni za Kiislamu

ShuleMadrasa
TauhidiFalsafaMaadili
Sayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
Uchumi
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

Uislamu na dini nyingine
Hofu ya Uislamu

Wasunni ni dhehebu kubwa ndani ya dini ya Uislamu. Takriban asilimia 80 - 90 za Waislamu wote duniani hukadiriwa kuwa Wasunni na wengine 10-20 % huhesabiwa kati ya Washia.

Wasunni huitwa kwa Kiarabu ahl ul-sunna (Kiarabu: أهل السنة; "watu wa mapokeo"). Neno Sunni hutokana na neno sunna (kwa Kiarabu : سنة ) inayomaanisha mapokeo ya Mtume Muhammad.

Isipokuwa Uajemi, Iraki, Bahrain, Azerbaijan, Yemen, Omani na Lebanoni kundi hilo ni kubwa katika nchi zote penye Waislamu wengi.

Historia

Wasunni hufuata mwelekeo wa Uislamu ulioanzishwa na ukhalifa wa Abu Bakr na kutokubali uongozi wa familia ya Mtume Muhammad kupitia Ali, Hassan na Husain.

Madhehebu ya Wasunni

Kati ya Wasunni kuna madhehebu nne zinazotofautiana kiasi kuhusu mafundisho ya sharia au sheria ya kidini ya Kiislamu. Ndio Wahanafi, Wamaliki, Washafii na Wahanbali. Kwa jumla Wasunni hukubaliana ya kwamba madhehebu haya yote manne ni sawa.

Walimu wengine hasa katika kikundi cha Wawahabi kilichoanzishwa kati ya Wahanbali kimekaza mafundisho yake hadi kuwashtaki wengine kuwa si Waislamu wa kweli.

Viungo vya Nje