Omani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
سلطنة عُمان
Sulṭanat ʿUmān

Usultani wa Omani
Bendera ya Omani Nembo ya Omani
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: (hakuna)
Wimbo wa taifa: Nashid as-Salaam as-Sultani
Lokeshen ya Omani
Mji mkuu Maskat
23°61′ N 58°54′ E
Mji mkubwa nchini Muskat
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali Ufalme
Qaboos bin Said Al Said
{{{sovereignty_type}}}
Waosmani kufukuzwa
1741
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
309,500 km² (ya 70)
(kidogo sana)
Idadi ya watu
 - Julai 2015 kadirio
 - 2010 sensa
 - Msongamano wa watu
 
3,286,9361 (ya 129)
2,773,479
13/km² (ya 216)
Fedha Rial (OMR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+4)
(UTC+4)
Intaneti TLD .om
Kodi ya simu +968

-

1Ndani ya idadi ya wakazi kuna watu 577,293 wasio raiaRamani ya Omani

Usultani wa Omani (kwa Kiarabu:سلطنة عُمان Saltanat ˤUmān) ni nchi ya Bara Arabu katika Asia ya Magharibi.

Imepakana na Maungano ya Falme za Kiarabu, Saudia na Yemen, halafu Bahari Hindi na Ghuba ya Omani.

Utawala wa nchi hufuata muundo wa kifalme usiobanwa na masharti ya katiba.

Mji mkuu ni Maskat (Omani).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Omani ilikuwa kituo muhimu cha biashara kwenye Bahari Hindi na Ghuba ya Uajemi tangu milenia mbili KK.

Tangu kuja kwa Uislamu Omani ilikuwa ama chini ya Uajemi au chini ya khalifa wa Baghdad na baadaye Dola la Seljuki.

Kati ya miaka 1507 na 1650 mji wa Maskat na pwani ya Omani vilitawaliwa na Ureno.

Makabila ya bara yaliunganika chini ya maimamu wa madhehebu ya Kiislamu ya Waibadiya na Imam Nasir ibn Murshid († 1649) alifaulu kupunguza eneo la Wareno. Mfuasi wake Sultan ibn Saif aliwafukuzwa Wareno kabisa na kushambulia vituo vyao kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki.

Masultani wa Omani walitawala pwani ya Afrika ya Mashariki katika karne ya 19. Mwaka 1830 Sultani Sayyid Said alihamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja mji wa Zanzibar (Unguja). Baada ya kifo chake mwaka 1856 dola liligawiwa kuwa nchi mbili:

Mnamo 1890 Omani ilikuwa eneo lililogawiwa kati ya Sultani wa Maskat na Imamu wa Ibadiya.

Maskat ilikubali kuwa eneo lindwa chini ya Uingereza ikapata msaada wa jeshi la Uingereza dhidi ya Saudia na baadaye kuvamia na kutawala pia maeneo ya imamu mwaka 1957.

Mkataba wa mwaka 1951 ulitangaza uhuru wa Omani, lakini hali halisi athira ya Uingereza ulikuwa na nguvu hadi miaka ya 1990.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wengi ni Waarabu, Wabeluchi, Wahindi, Waafrika n.k. Zaidi ya asilimia 40 ni wahamiaji.

Wenyeji karibu wote ni Waislamu, wakati wageni ni wa dini nyingi tofauti.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiarabu, lakini Kibeluchi, Kiurdu na Kiingereza pia vinatumika sana.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Kirgizstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Omani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.