Afya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Stempu ya posta ya New Zealand, mnamo mwaka 1933.
Mwanamke akinawa mikono 1655 hivi.
Donald Henderson na wenzake katika kukinga watu dhidi ya ndui mwaka 1966.

Afya ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili, kiroho na kiutu pia, bila kusumbuliwa na ugonjwa wowote.

Afya ya binadamu itakuwa njema kama atafuatilia kanuni na taratibu bora za afya. Hiyo inajumuisha mlo kamili, yaani chakula chenye virutubisho vyote, vikiwemo protini, wanga na fati (hiyo iwe katika asilimia ndogo sana).

Pia anatakiwa awe safi kimwili na kimazingira, kama vile kwa kuoga na kusafisha mazingira yanayomzunguka.

Pia tunatakiwa kuwa na afya ya kiroho yaani kuishi kadiri ya mafundisho ya Mwenyezi Mungu kama vile: kupendana, kuthaminiana na kuacha dhambi: mara nyingi hizo zinadhuru afya ya mwili pia.

Fafanuzi za afya[hariri | hariri chanzo]

Sawa na suala la ugonjwa, hakuna elezo kamili kuhusu hali ya afya.

  • Kwa watu wengi ni hali ya kutosumbuliwa na maumivu na udhaifu, pamoja na uwezo wa kutumia sehemu zote za mwili. Ni wazi ya kwamba hisia hii ni tofauti kati ya mtu na mtu.

Majukumu[hariri | hariri chanzo]

Serikali zinatarajiwa kuandaa wataalamu wa mambo ya afya na kujenga hospitali nyingi hata vijijini kwa sababu watu wengi hupoteza maisha kwa kukosa huduma za afya: hii itasaidia kupunguza vifo.

Watu wanatakiwa kuwa na ustadi wa kufanya mazoezi kwa wingi. Hata mjamzito anapaswa kufanya mazoezi, ingawa si kazi ngumu.

Pia kula mlo bora wakati wote ili kuepukana na magonjwa yanayotokana na ukosefu wa chakula fulani (virutubishi).

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.who.int/bulletin/archives/80(12)981.pdf ''WHO definition of Health''

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Wikiquote-logo.svg
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Rod of Asclepius2.svg Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Afya kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.