Nenda kwa yaliyomo

Mtaalamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wataalamu)
Wataalamu watatu wa nyota katika Injili ya Mathayo, kanisa kuu la Cologne, Ujerumani.

Mtaalamu (kutoka neno la Kiarabu lenye mzizi mmoja na neno 'elimu') mara nyingi humaanisha mtu ambaye ni bingwa katika taaluma fulani.

Mtaalamu anaaminika katika fani yake kama chanzo cha ujuzi au maarifa.

Utaalamu huo unaweza kutegemea elimu, lakini pengine pia malezi, ufundi, maandishi au mang'amuzi yake.

Kihistoria, mtaalamu aliweza kuitwa mzee wa hekima.

Mtu huyo kwa kawaida alikuwa na uwezo mkubwa upande wa akili pamoja na busara katika maamuzi.[1]

Mfano; mtaalamu wa lugha za alama, mtaalamu wa kuchora picha, mtaalamu wa kutunga mashairi ya nyimbo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]