Kanisa kuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kanisa kuu

Kanisa kuu ni jina la heshima la jengo la ibada la Ukristo ambalo Askofu wa jimbo (dayosisi) fulani analitumia kwa kawaida kutekeleza kazi yake kama mchungaji mkuu wa waamini wake.

Jina hilo linashuhudiwa tayari na maandishi ya mwaka 516.

Linaitwa pia "kanisa mama" kwa sababu ni kama mama ya makanisa yote ya jimbo hilo.

Ndani yake umo ukulu, yaani kiti cha Askofu kisichopatikana katika makanisa mengine.