Basilika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Basilika.

Basilika ni jina la heshima kwa ajili ya kanisa fulani katika Kanisa Katoliki.

Muundo wa basilika hii unaonyesha ukumbi kuu katikati na kumbi za kando kati ya nguzo na ukuta

Asili ya basilika[hariri | hariri chanzo]

Kwa asili lilikuwa jengo rasmi lililotumika huko Roma ya Kale kama mahali pa mikutano ya hadhara na maamuzi ya kimahakama.

Jina ni la Kigiriki (aulè basilikè, yaani ukumbi wa kifalme), hivyo linaelekeza kuona asili ya majengo hayo upande wa mashariki wa Bahari ya Kati

Basilika kama jengo la kanisa[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia mwaka 313, Dola la Roma liliporuhusu raia kufuata Ukristo, basilika ziligeuzwa kuwa mahali pa ibada ya dini hiyo, kuanzia Kanisa kuu la Roma, maarufu kwa jina la Mt. Yohane huko Laterani.

Baadaye zikajengwa Basilika la Mt. Petro huko Vatikani, Basilika la Bikira Maria Mkuu na Basilika la Mt. Paulo nje ya kuta za jiji.

Baadaye, cheo cha Basilika kilitolewa kwa makanisa mengi mengi kutokana na umuhimu wake upande wa historia, dini na sanaa.

Hata hivyo, kuna basilika kuu na basilika dogo.

Muundo wa basilika yenye kumbi 5

Basilika kama mfumo wa pekee wa ujenzi[hariri | hariri chanzo]

Katika fani ya historia ya usanifu ni jina kwa ajili ya kanisa liliyojengwa kwa kufuata mfumo wa pekee. Hapu kanisa huwa na ukumbi kuu na kando lake sehemu ya pembeni inayotengwa kwa nguzo. Mara nyingi muundo huu ulikuwa na kumbi mbili za kando lakini kuna pia basilika kubwa zenye kumbi 2 za kando kila upande kwa hiyo jumla 5.

Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Basilika kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.