Helsinki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru







Helsinki

Nembo
Majiranukta: 60°10′N 26°56′E / 60.167°N 26.933°E / 60.167; 26.933
Nchi
Kaunti Helsinki
Idadi ya wakazi (2013)
 - Wakazi kwa ujumla 610 601
Tovuti:  www.hel.fi
Helsinki
Helsinki mjini
Wilaya ya Kalasatama na skyscrapers huko Helsinki mnamo Machi 2021
Itäkeskus

Helsinki (kwa Kiswidi: Helsingfors) ni mji mkuu wa Ufini na pia mji mkubwa nchini. Idadi ya wakazi ni 610,601 (2013) na kuna jumla ya milioni moja katika rundiko la mji.

Jiografia

Helsinki iko kwenye mwambao wa Ghuba ya Ufini ya bahari ya Baltiki; imesambaa mwambaoni wa hori mbalimbali na visiwa vya Ghuba hiyo.

Historia

Manmo 1550 eneo la Helsinki lilikuwa sehemu ya Uswidi na mfalme wa Uswidi Gustav Vasa aliamuru kujengwa kwa mji mpya. Lakini wakati wa utawala wa Uswidi mji ulioitwa kwa Kiswidi "Helsingfors" haukuendela sana.

Tangu mwaka 1809 Ufini ilikuwa chini ya utawala wa Urusi na Kaisari Alexander I wa Urusi aliamuru kuhamisha mji mkuu wa jimbo hili kwenda Helsinki na kujenga mji upya. Tangu wakati ule Helsinki imekua kushinda mji wa Turku uliowahi kuwa mji mkubwa katika Ufini hadi wakati ule.

Tangu mwaka 1917 Helsinki imekua mji mkuu wa nchi mpya ya Ufini.

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Ufini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Helsinki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.