Thenashara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Thenashara (pia thinashara) ni Kiswahili cha pwani kwa ajili ya namba kumi na mbili (12).

Asili ni Kiarabu "اثنا عشر" (ithnayn `ashara - ithnashara).

Kwa Kiswahili sanifu "kumi na mbili" imechukua nafasi yake lakini bado hutumika.

Thenashara katika Biblia[hariri | hariri chanzo]

Katika tafsiri kadhaa za Biblia "Thenashara" inamaanisha Mitume wa Yesu kumi na wawili kama neno la Kigiriki "dodeka" (=12) linatumiwa kama jina si namba. Toleo la Biblia (Union Version) linatumia "wale Thenashera" pale ambako Kigiriki asilia cha Agano jipya kinasema "οἱ δώδεκα" (hoi dodeka) [1]. Pale ambako lugha asilia inatumia "dodeka" kama namba Kiswahili cha Union Version kinatumia "kumi na wawili".[2]

Matoleo mengine ya Biblia kwa mfano Habari Njema kwa watu wote hutumia "kumi na wawili" kote.


Thenashara katika Uislamu[hariri | hariri chanzo]

Wakati mwingine Thenashara inaweza kumaanisha dhehebu la Shia katika Uislamu ambalo mara nyingi kwa Kiarabu huitwa "Ithnashara" kutokana na maimamu 12 wanaoheshimiwa. Ni kundi kubwa kati ya Washia hasa nchini Uajemi, Irak na Lebanon.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. mifano: Mt 10:5, 20:17, 26:14, 26:47; Mk 3:16, Luka 8:1 na penginepo
  2. Mifano: Mt 10:1, 26:20, Mk 3:14 na penginepo