Nenda kwa yaliyomo

Biblia (Union Version)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Biblia (Union Version) ni tafsiri maarufu ya Biblia ya Kikristo katika lugha ya Kiswahili iliyotolewa mwaka 1953 kwa kuunganisha tafsiri za awali katika Kiunguja na Kimvita ili kupunguza gharama.

Ingawa hadi leo zimetolewa tafsiri nyingine za kisasa zaidi, kama vile Biblia Habari Njema iliyoandaliwa na Wakatoliki na Waprotestanti pamoja ili kurahisisha wasomaji wa wakati huu kuelewa ujumbe kwa urahisi zaidi, bado Biblia (Union Version) inatumika sana kwa sababu ya kufuata kwa karibu maneno yenyewe ya lugha asili za Biblia: Kiebrania, Kiaramu na Kigiriki.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Biblia (Union Version) kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.