Kanisa kuu la Roma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kama majimbo yote ya Kanisa Katoliki, jimbo la Roma, ambalo askofu wake ni mkuu wa maaskofu wote, lina jengo moja la ibada linaloheshimiwa kama ishara ya umoja wa waamini wake.

Likiwa kanisa kuu la Papa, papo hapo ni kanisa kuu la dunia nzima kwa Wakristo wenye ushirika kamili naye.

Tangu karne ya 4 hadi leo kanisa hilo liko katika mtaa wa Laterani.

Liliwekwa wakfu mwaka 314 kwa heshima ya Kristo Mkombozi, lakini linajulikana zaidi kwa jina la Mt. Yohane (Mbatizaji), msimamizi wa Roma.

Katika kanisa hilo mara tano ulifanyika mtaguso mkuu.