Ushirika kamili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ushirika kamili ni msamiati wa teolojia ya [Ukristo]] kuhusu Kanisa.

Unamaanisha umoja kamili kati ya madhehebu mbalimbali kwa msingi wa imani ileile inayoyawezesha kushirikiana kikqamilifu katika ibada na hasa ekaristi na sakramenti nyingine.[1]

Unatumika hasa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa mashariki, ukitofautishwa na ushirika usio kamili au wa kiasi tofautitofauti uliopo kati ya Wakristo wa aina zote kadiri wanavyozidi kusadiki mambo yaleyale ya msingi zaidi (kama vile Utatu mtakatifu, umungu wa Yesu Kristo na ufufuko wake), ingawa wanapishana katika mengine (hasa Kanisa na sakramenti]].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. On Receiving Anglican clergy into the Catholic Church; How to become a Catholic Archived Juni 11, 2009 at the Wayback Machine.; When an Orthodox joins the Catholic Church Archived Agosti 31, 2009 at the Wayback Machine.;On Participants in RCIA and Confirmation Archived Septemba 24, 2015 at the Wayback Machine.; My Return to the Catholic Church; etc.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christianity Symbol.png Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ushirika kamili kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.