Mtaguso wa nne wa Laterano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Basilika la Mtakatifu Yohane huko Laterano ambamo mtaguso ulifanyika.

Mtaguso wa nne wa Laterano (1215) unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na mbili.

Uliitishwa na Papa Inosenti III (1198-1216) kama kilele cha kazi yake.

Ulihudhuriwa na maaskofu zaidi ya 400 (wakiwemo mapatriarki wa Kilatini wa Konstantinopoli na Yerusalemu na wawakilishi wa wale wa Antiokia na Aleksandria), na wakuu wa watawa zaidi ya 800, mbali na mabalozi wa watawala wa nchi mbalimbali.

Mada kuu zilikuwa Vita vya msalaba, Mashindano kuhusu uteuzi wa viongozi wa Kanisa, mamlaka ya Papa, mwenendo wa makleri, mashirika ya kitawa, imani (kuhusu ekaristi n.k.), na wajibu wa Wakristo wote kupokea sakramenti ya kitubio walau mara moja kwa mwaka.

Kutokana na wingi na umuhimu wa mafundisho na maamuzi yaliyotolewa, mtaguso huo unahesabiwa kuwa kati ya ile iliyoathiri zaidi Kanisa hadi leo.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mtaguso uliitishwa mjini Roma na Papa Inosenti III kwa hati Vineam Domini Sabaoth, iliyotolewa tarehe 19 Aprili 1213.

Papa mwenyewe ndiye aliyefungua kikao kwa hotuba ya kusisimua tarehe 11 Novemba 1215, naye tarehe 30 Novemba alipendekeza kanuni 70 ambazo zilipitishwa bila ya kupingwa.

Hivyo mtaguso huo ulizidi kukusanya mamlaka ya Kanisa mikononi mwa Papa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtaguso wa nne wa Laterano kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.