Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli uliitishwa na kaisari Justiniani I mwaka 553 kwa lengo la kupatanisha tena na Kanisa Katoliki Wakristo wote wa Misri, Syria n.k. waliojitenga miaka 100 iliyopita kufuatana na Mtaguso wa Kalsedonia.

Kwa ajili hiyo kaisari huyo alifanya yalaaniwe maandishi ya Wanestori watatu (Teodoro wa Mopsuestia, Theodoreto wa Kuro na Iba wa Edesa) yaliyochukiwa sana na Wamisri.

Pia mtaguso mkuu huo ulilaani baadhi ya mafundisho wa Origene.

Walihudhuria maaskofu 168; kati yao 11 walitokea magharibi. Kumbe Papa Vigili (537-555), pamoja na maaskofu wengine 12 wa magharibi walikataa kuhudhuria ingawa walikuwepo Konstantinopoli, ila mwaka uliofuata alikubali maamuzi ya mtaguso.

Hatimaye Papa Gregori I (590-604) aliutambua kama mtaguso mkuu kwa sababu haukuharibu kitu. Hivyo Wakristo wengi wanahesabu mtaguso huo kuwa wa tano kati ya Mitaguso ya kiekumeni, ingawa lengo halikufikiwa, kwa kuwa Wamisri waliendelea kukataa mtaguso wa Kalsedonia.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.