Mtaguso wa Yerusalemu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mtaguso wa Yerusalemu au Mtaguso wa mitume ni jina linalotumika kwa mkutano uliofanyika mwaka 49 au 50 ili kuondoa tofauti za misimamo kati ya Wakristo kuhusu wajibu wa kutekeleza Torati kwa waongofu waliotokea upagani.

Ni kwamba Mtume Paulo na Mtume Barnaba waliporudi Antiokia kutoka safari yao ya kwanza ya kimisionari walipaswa kupambana na Wakristo wa Kiyahudi kuhusu uwezekano wa mataifa kuokoka pasipo kutahiriwa.

Hatimaye suala likapelekwa Yerusalemu kwa Kanisa mama. Baada ya majadiliano marefu Mtume Petro akatoa neno la mwisho kwamba Wapagani wanaomuamini Yesu Kristo wasitwishwe mzigo usiobebeka wa kufuata sheria za Kiyahudi (Mdo 15:1-12).

Katika Gal 2:1-10 Paulo pia ametuachia kumbukumbu ya mtaguso huo akisisitiza kuwa mitume waliokuwepo (Yakobo Mdogo, Petro na Yohane) walitambua rasmi karama ya kimisionari ya kwake na ya Barnaba na uhalali wake, wakiwaomba tu wachangishe pesa kati ya Wakristo wa mbali kwa ajili ya wenzao wa Yerusalemu wenye hali ngumu. Hiyo ilikuwa namna mpya ya kutekeleza upendo wa kidugu na kudumisha umoja wa Kanisa baada ya uenezi wake.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtaguso wa Yerusalemu kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.