Nenda kwa yaliyomo

Yakobo Mdogo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha yake iliyochorwa katika ukuta wa kanisa la Waorthodoksi huko Vladimir, Russia karne ya 12.
Mitume wa Yesu
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho   Utoto wa Yesu   Ubatizo   Arusi ya Kana   Utume wa Yesu   Mifano ya Yesu   Miujiza ya Yesu   Kugeuka sura   Karamu ya mwisho   Msalaba wa Yesu   Maneno saba   Kifo cha Yesu   Ufufuko wa Yesu   Kupaa mbinguni   Ujio wa pili  Yesu na matabiri ya Agano la Kale   Injili   Majina ya Yesu katika Agano Jipya   Yesu kadiri ya historia   Tarehe za maisha ya Yesu   Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi   Kiaramu   Bikira Maria   Yosefu (mume wa Maria)   Familia takatifu   Ukoo wa Yesu   Ndugu wa Yesu   Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya  · Mitazamo ya Kikristo   Mitazamo ya Kiyahudi   Mitazamo ya Kiislamu   Yesu katika sanaa

Yakobo Mdogo ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu. Anaitwa hivyo ili kumtofautisha na mtume mwenzake, Yakobo wa Zebedayo.

Katika Injili anaitwa Yakobo wa Alfayo na kutajwa na Injili ya Mathayo 10:3, Injili ya Marko 3:18, Injili ya Luka 6:15, mbali ya Matendo ya Mitume 1:13.

Kutokana na wingi wa Wayahudi waliotumia jina hilo la babu wa taifa la Israeli, ni vigumu kuelewa kama ndiye Yakobo anayetajwa kama mmoja kati ya nguzo za Kanisa la Yerusalemu aliyekubali pendekezo la Mtume Petro kuhusu suala la tohara kwa wasio Wayahudi wanaoongokea Ukristo na hasa kama ndiye mwandishi wa Waraka wa Yakobo [1].

Kama ndiye, aliuawa Yerusalemu mwaka 62 kwa himizo la kuhani mkuu Anna II.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Mei pamoja na Mtume Filipo [2][3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/21000
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/94044
  • Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 155
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 132
  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 39
  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 81-82

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yakobo Mdogo kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.