Nenda kwa yaliyomo

Mtume Thoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kifodini cha Mtume Thomas kilivyochorwa na Peter Paul Rubens.
Mitume wa Yesu
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho   Utoto wa Yesu   Ubatizo   Arusi ya Kana   Utume wa Yesu   Mifano ya Yesu   Miujiza ya Yesu   Kugeuka sura   Karamu ya mwisho   Msalaba wa Yesu   Maneno saba   Kifo cha Yesu   Ufufuko wa Yesu   Kupaa mbinguni   Ujio wa pili  Yesu na matabiri ya Agano la Kale   Injili   Majina ya Yesu katika Agano Jipya   Yesu kadiri ya historia   Tarehe za maisha ya Yesu   Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi   Kiaramu   Bikira Maria   Yosefu (mume wa Maria)   Familia takatifu   Ukoo wa Yesu   Ndugu wa Yesu   Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya  · Mitazamo ya Kikristo   Mitazamo ya Kiyahudi   Mitazamo ya Kiislamu   Yesu katika sanaa

Thoma (au Didimo, yaani Pacha) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa kama mtakatifu, kwa namna ya pekee na Wakristo wa maeneo yaliyokuwa mashariki kwa Dola la Roma, kuanzia Iraq hadi India.

Inawezekana kwamba sababu yake ni kazi za utume alizozifanya huko hadi kifodini chake huko Chennai mwaka 72 (kaburi lake huonyeshwa katika mji huo wa Tamil Nadu). Mpaka leo kusini-magharibi mwa Bara Hindi wako wanaojiita "Wakristo wa Thoma" ambao kwa muda mrefu walikosa mawasiliano na Wakristo wengine wa mbali.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na madhehebu mengine mbalimbali kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 3 Julai[1].

Chanzo cha umaarufu wake

[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa mtu mwenye tabia ya pekee iliyomvutia umaarufu hadi leo. Hasa alielekea kukata tamaa, kupinga hoja na kutosadiki kwa urahisi, kama alipokataa kusadiki ushahidi wa mitume wenzake juu ya ufufuko wa Yesu[2].

Mfano mmojawapo ni pale ambapo katika karamu ya mwisho alimjibu Yesu kwa wasiwasi: "Bwana, hatujui uendako; tutajuaje basi njia?" (Yoh 14:5). Ndipo Yesu alipojitambulisha kama njia: "Mimi ndimi njia, ukweli na uzima" (Yoh 14:6).

Hata hivyo, Injili ya Yohane ambayo ndiyo inayomzungumzia zaidi katika Biblia ya Kikristo, inaripoti jibu lake la mwisho kwa Yesu mfufuka kama ifuatavyo (Yoh 20:28): "Bwana wangu na Mungu wangu!" Katika Injili hakuna ungamo la wazi zaidi la umungu wa Yesu Kristo.

Hata hivyo, Yesu alimuambia wana heri zaidi wanaosadiki bila kuona kwanza. Na ndilo lengo la Yohane katika kuandika Injili yake: kuwafanya wasomaji wasioweza tena kumuona Yesu wamuamini na hivyo kupata uzima wa milele [3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Martyrologium Romanum
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/21150
  3. Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 217-219
  • Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 230-231
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 194-195
  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 54

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtume Thoma kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.