Mitazamo ya Kiyahudi juu ya Yesu
Mitazamo ya Kiyahudi juu ya Yesu ni ya aina mbalimbali, lakini yote haimkubali, la sivyo ingewabidi wahusika wamuamini na kubatizwa badala ya kuendelea na dini yao ambayo viongozi wake walimhukumu ni kafiri anayestahili kuuawa.
Kwa kawaida Wayahudi wanamuona Yesu kama mmojawapo kati ya wengi waliojinadi kuwa Masiya katika nyakati mbalimbali za historia ya taifa lao.[1]
Yesu anatazamwa kama yule aliyefaulu zaidi kukubalika, na kwa sababu hiyo, kuleta madhara makubwa kuliko wote.[2]
Uyahudi haujawahi kumkubali rasmi Masiya yeyote kuwa ametimiza utabiri wa manabii. Zaidi ya hayo, unaona ibada ya Wakristo kwa Yesu kuwa kinyume cha imani katika Mungu mmoja tu.[3]
Katika Karne za Kati, Judah Halevi na Maimonide walimuona Yesu (kama vile Muhammad) kama mtu muhimu katika kuandaa mataifa yote kwa ujio wa Masiya atakayeyafanya yamuabudu Mungu pekee.
Siku hizi kuna wataalamu Wayahudi wanaosema Yesu alikuwa jirani na dini yao kuliko Injili zinavyoonyesha. Mtazamo huo ulianzishwa katika karne ya 18 na Jacob Emden na Moses Mendelssohn.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mitazamo ya Kiyahudi juu ya Yesu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Jesus of Nazareth
- ↑ Maimonides. Mishneh Torah, Sefer Shofetim, Melachim uMilchamot, Chapter 11, Halacha 4. Chabad translation by Eliyahu Touge.
- ↑ Devarim (Deuteronomy) 6:4