Nenda kwa yaliyomo

Yosefu (mume wa Maria)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Arusi ya Bikira Maria ya Perugino.
Familia takatifu pamoja na Roho Mtakatifu walivyochorwa na Murillo, 1675-1682.
Mt. Yosefu akiwa usingizini alivyochorwa na Gentile da Fabriano.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Yosefu (kwa Kiebrania יוֹסֵף, "Yosef"; kwa Kigiriki Ἰωσήφ), kadiri ya Injili, alikuwa mume wa Bikira Maria na baba mlishi wa Yesu Kristo ambao pamoja naye waliunda Familia takatifu.

Injili ya Mathayo (13:5) inamsifu kwa uadilifu wake na kumtaja kama "fundi" (kwa Kigiriki téktón). Lakini inasema pia (sawa na Injili ya Luka) kuwa alitoka katika ukoo wa mfalme Daudi. Ndiye aliyetunza familia hiyo kwa kazi ya mikono yake na kumfundisha mtoto Yesu kufanya kazi za kibinadamu.

Injili na imani ya Kikristo zinasisitiza kuwa baba halisi wa Yesu alikuwa Mungu mwenyewe: Maria alimchukua mimba kwa muujiza uliosababishwa na Roho Mtakatifu.

Ndoto ya Mt. Yosefu, mchoro wa Josè Luzan

Yosefu, kisha kujulishwa juu ya mimba hiyo, alikubali kumchukua mchumba wake nyumbani na kumtambua mwanae kuwa ni wa kwake ingawa hakuwahi kujamiiana naye. Hivyo alitunza heshima ya mama na mtoto na kuwahakikishia ulinzi katika jamii inayojali zaidi wanaume.

Miezi baadaye yeye na Maria walikwenda Bethlehemu kwa ajili ya sensa, na ndipo Yesu alipozaliwa pangoni na kulazwa horini.

Wakati huo Yosefu alishuhudia ujio wa wachungaji waliokuja kumuabudu mtoto kadiri ya tangazo la malaika waliowatokea.

Kadiri ya Torati ya Musa, siku nane baada ya mtoto kuzaliwa, Yosefu alimpa mtoto jina wakati wa kutahiriwa, na siku arubaini baadaye alimpeleka hekaluni Yerusalemu ili kumtolea Mungu kama mtoto wa kiume wa kwanza. Ndipo wazee Simeoni na Anna binti Fanueli walipotoa utabiri juu ya Yesu.

Baada ya mamajusi kuwatembelea Bethehemu, wanafamilia walikimbilia Misri ili kukwepa dhuluma ya mfalme Herode Mkuu aliyetaka kumuua mtoto kwa kuogopa atampindua baadaye.

Kisha wakarudi Nazareti (Galilaya) ambapo Yesu alikua vizuri chini ya wazee wake.

Yesu alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote watatu walikwenda kuhiji Yerusalemu kwa Pasaka. Wakati wa kurudi, mtoto alibaki mjini akapatikana tena siku ya tatu akiwa hekaluni kati ya walimu wa sheria, akitokeza hekima yake. Alipoulizwa na Maria kuhusu mwenendo wake, mtoto alionyesha kujitambua si mwana wa Yosefu, bali wa Mungu. Hata hivyo alizidi kumheshimu na kumtii yeye kama baba pamoja na Mama Maria.

Baada ya taarifa hiyo, hakuna tena habari juu ya Yosefu, hivi kwamba wengi wanajiuliza kuhusu kifo chake na kuhisi kilikuwa kimeshatukia Yesu alipoanza utume wake.

Heshima baada ya kifo

[hariri | hariri chanzo]

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Heshima hiyo ilizidi kukua hasa magharibi kadiri ulivyozingatiwa ubinadamu wa Yesu.

Hatimaye alitangazwa na Mapapa kuwa msimamizi wa Kanisa lote kwa jinsi alivyosimamizi vizuri familia takatifu na katika karne ya 20 na ya 21 jina lake limeingizwa katika sala za ekaristi zote za liturujia ya Roma.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Machi, mbali ya kumbukumbu yake kama mfanyakazi tarehe 1 Mei iliyoongezwa na Papa Pius XII mwaka 1955 ili kuwapa kielelezo na msimamizi wafanyakazi Wakristo wanaosherehekea siku hiyo pamoja na wenzao wa sehemu nyingi za dunia Sikukuu ya kazi [1].

Katika muziki

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Mt. Yosefu (Mariahilfer Kirche, Vienna, Austria).

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yosefu (mume wa Maria) kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.